Ni kauli yake Waziri wa mifugo Mh Luhaga Mpina, alipozuru banda la Kinondoni lililopo viwanja vya Tungi Mkoani Morogoro, katika maonesho ya 25, ya Nane nane, kwa lengo la kuangalia utekelezaji wa kauli mbiu ya mwaka huu isemayo "Wekeza katika kilimo, mifugo na uvuvi kwa maendeleo ya viwanda "
Katika ziara yake hiyo aliyopokelewa na mwenyeji wake ambaye ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Ndg Aron T. Kagurumjuli, Baraza la Madiwani, wakuu wa idara na vitengo kutoka Manispaa hiyo, pia amepata fursa ya kutembelea maeneo tofauti tofauti ya Kilimo, mifugo na uvuvi ambapo Kinondoni imetekeleza kwa vitendo.
Mh Mpina ameambatana na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh Kebwe Steven Kebwe, Mama Theresia Mmbando ambaye kwa sasa ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani, pamoja na viongozi wengine wa vyama na Serikali.
Imeandaliwa na
Kitengo cha Uhusiano na Habari.
Manispaa ya Kinondoni.
Dar es salaam, Tanzania
Postal Address: P.O.BOX 31902 ,2Morogoro Road
Namba za simu: +255 22 2170173
Namba ya simu :
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz