Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam imetoa wito kwa Halmashauri za Mkoa wa Dar es Salaam kuhamasisha watumishi, watendaji na wananchi ndani na nje ya nchi , kutembelea vivutio mbalimbali vilivyopo Jijini Dar es salaa kama vile Majengo ya kale kupata historia ya jiji la Dar es salaam, pamoja na vivutio vya kiutamaduni na vile vya bahari ya Hindi.
Hatua hii inakusudia kuhamasisha ukuaji wa utalii jijini Dar es salaam, ili Jiji litambulike kati ya Majiji ya kitalii Duniani.
Ili kutimiza azma hii, watumishi na wageni wote wa ndani na nje ya Nchi wanahamasishwa kutembelea vivutio hivyo kwa gharama nafuu.
Imeandaliwa na
Kitengo cha Uhusiano na Habari.
Manispaa ya Kinondoni.
Dar es salaam, Tanzania
Postal Address: P.O.BOX 31902 ,2Morogoro Road
Namba za simu: +255 22 2170173
Namba ya simu :
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz