KATA YA MWANANYAMALA.
Kata ya Mwananyamala ilianza mnamo mwaka 1999, na ni Kata ambayo imepakana na Kata ya Kinondoni, Hanansif, Magomeni, na Mikocheni.
Jina la Mwananyamala limetokana na Lugha ya Kizaramo linalomaanisha "MTOTO NYAMAZA"
MITAA INAYOUNDA KATA HII.
Kata hii inaundwa na Jumla ya Mitaa saba kama ifuatavyo:-
1. Mtaa wa Kambangwa
2. Mtaa wa Kopa.
3. Mtaa wa Misisiri A.
4. Mtaa wa Misisiri B.
5. Mtaa wa Msolomoni.
6. Mtaa wa Bwawani.
7. Mtaa wa Mwinjuma.
UONGOZI WA KATA.
Diwani wa Kata ya Mwananyamala ni Mh.Songoro Mnyonge.
Diwani wa Viti Maalumu ni Rose Moshi.
Uongozi wa Kata ya Mwananyamala umekamilika vizuri na wanashirikiana pamoja na wenyeviti wa Mitaa katika kuleta Maendeleo.
MIRADI KATA INAYOJIVUNIA.
• Mradi wa Jengo la Bima ya Afya Mwananyamala hospital-VIP WARD.
• Mradi wa kuboresha jengo la Mochwari.
• Mradi wa Mfereji wa maji ya mvua unaoanzia Mwananyamala "A” hadi Komakoma.
• Mradi wa ujenzi wa Madarasa ya shule ya Sekondari Kambangwa.
HALI YA ELIMU.
Kata ya Mwananyamala ina taasisi mbalimbali zinazotoa elimu zikiwemo shule za awali, Msingi na Sekondari. Shule za Msingi za Serikali ni nne nazo ni:-
• Shule ya Msingi Mwongozo.
• Shule yaMsingi Kinondoni.
• Shule yaMsingi Msisiri B
• Shule ya Msingi Msisiri.
SHULE YA SEKONDARI YA SERIKALI.
Shule ya Sekondari Kambangwa.
HALI YA AFYA KATIKA KATA.
Hali ya Afya na Usafi inaridhisha katika Kata hii, na ni kutokana na vikundi vya uzoaji taka ambavyo vinazoa taka katika Mitaa iliyopo katika Kata ya Mwananyamala.
Dar es salaam, Tanzania
Postal Address: P.O.BOX 31902 ,2Morogoro Road
Namba za simu: +255 22 2170173
Namba ya simu :
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz