KATA YA MSASANI.
Kata ya Msasani kwa asili ya Jina lake inasadikiwa kuwa ni kutokana na Mtu maarufu aliyeishi maeneo hayo kipindi hicho aitwaye Mussa Hassan , na kutokana na wenyeji wa eneo (Wamakonde), kushindwa kutamka kwa usahihi jina hilo na mwisho kutamka Msasani.
IDADI YA MITAA ILIYOPO KWENYE KATA
Kata ya Msasani ina mitaa Mitano kama ifuatavyo:-
1. Mtaa wa Oysterbay
2. Mtaa wa Masaki
3. Mtaa wa Bonde la Mpunga
4. Mtaa wa Makangira
5. Mtaa wa Mikoroshoni.
Diwani wa Kata ni Benjamini Kawe Sitta.
Diwani Viti Maalumu ni Tatu Maliaga.
Honoratha Mashoto.
HALI YA ELIMU KATIKA KATA.
SHULE ZA MSINGI ZA SERIKALI.
Kata ya Msasani inazo shule za Msingi za Serikali tano ambazo ni
• Shule ya Msingi Msasani A.
• Shule ya Msingi Msasani B
• Shule yaMsingi Mbuyuni
• Shule ya Msingi Bongoyo.
• Shule ya Msingi Oyesterbay.
Shule zote hizi zinamiundo ya maji safi na Umeme. Shule ya Msingi Oyestrbay imepandishwa daraja na kuwa shule ya English Medium, Aidha kuna vitengo vya kuhudumia watoto wenye mahitaji maalumu(Disabilities), katika Shule ya Msingi Msasani A na Mbuyuni.
SHULE ZA MSINGI ZA BINAFSI.
Kata ya Msasani inazo pia shule za Msingi za Binafsi ambazo ni:-
• Shule ya Msingi ya Drive Inn Msasani Islamic
• Shule ya Msingi ya Penisula Good Sanitarian.
SHULE YA SEKONDARI YA SERIKALI.
Kata ya Msasani inayo shule moja ya Sekondari ambayo ni ya Serikali iitwayo Oysterbay Secondary School.
SHULE ZA SEKONDARI ZA BINAFSI.
Kata ya Msasani inazo pia Shule za Sekondari za Binafsi tano kama zifuatazo;-
• Sekondari ya Tanganyika International
• Sekondari ya Dar Es SalaamSchool
• Sekondari ya Good Sanitarian.
• Sekondari ya Islamic
• Sekondari ya Siera.
HALI YA AFYA.
Hali ya Afya katika Kata ya Msasani ni ya kuridhisha kwani inayo hazina ya kutosha ya hospital, vituo vya Afya pamoja na Zahanati, za Binafsi japo kuwa hakuna zahani ya Kata ya Serikali. Kata hii inayo hazina ya hospital za binafsi kama ifuatavyo:-
HOSPITAL ZA BINAFSI ZILIZOPO KATA YA MASASANI.
• Hospital ya Msasani Penisula.
• Hospital ya London.
• Hospital ya Santas
• Hospital ya Oysterbay
• Hospital Sali International
VITUO BINAFSI VYA AFYA VILIVYOPO KATA YA MSASANI.
• Kituo cha Afya cha ABC Dental Centre.
• Kituo cha Afya cha Aghakan Medical Centre.
• Kituo cha Afya cha ST lAURENT Diabetic Centre.
ZAHANATI BINAFSI ZILIZOPO KATA YA MSASANI
• Kidney Care
• TPM Dispensary
• Bonde la Mpunga Dispensary
• New Msasani Dispensary
• Oyster bay Dispensary.
• Sanitarian Dispensary
• St. Benedict Dispensary
• New Vision Eye Clinic
• Divine Grace Dental Clinic
• Letus physiotherapy Clinic
• Dental Studio Clinic
• Premier Care Clinic
• Elite Dental Clinic.
HALI YA MIUNDOMBINU YA BARABARA.
Asilimia 90%ya Barabara Katika Kata hii zimejengwa kwa kiwango cha Lami, asilimia 10% nibarabara za udongo.
USAFI WA MAZINGIRA.
Usafi wa Mazingira wa Kata hii ni wa kuridhisha kwani kila mtaa unao wakandarasi wa Usafi wanaozoa matakataka kwa wakati na hutumia mashine za EFD.
MAHUSIANO NA WADAU.
Mahusiano ya wadau wa maendeleo na uongozi wa Kata na Mitaa ni mzuri, kwani wako mstari wa mbele kuchangia shughuli za Kijamii na miradi ya Maendeleo.
MRADI WA KUJIVUNIA.
Mradi wa Kujivunia Katika Kata ya Msasani ni Ujenzi wa Mfereji Mkubwa wa maji ya mvua kutoka Mayfair hadi Baharini ambao unasaidia kuondoa kero ya Mafuriko katika Kata ya Masasani.
MIPANGOMIJI.
Kata ya Msasani eneo lake kubwa limepimwa na sehemu ndogo ya Makazi holela ambako hakujapimwa hivyo kupelekea watu kupima wenyewe kunakoleteleza changamoto ya miundombinu ya barabara za Mitaa.
Dar es salaam, Tanzania
Postal Address: P.O.BOX 31902 ,2Morogoro Road
Namba za simu: +255 22 2170173
Namba ya simu :
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz