HII HAPA KATA YA MAGOMENI.
Kata ya Magomeni ilianza mwaka 2000, asili ya jina la Magomeni ilitokana na hali ya kuwa na miti mikubwa iliyokuwa inatoa Magome, hali iliyopelekea watu wa sehemu tofauti na hapo kupaita Magomeni.
IDADI YA MITAA.
Mitaa inayounda Kata ya Magomeni ni mitano kama ifuatavo nayo ni:-
1. Mtaa wa Makuti A
2. Mtaa wa Makuti B
3. Mtaa wa Idrissa
4. Mtaa wa Suna
5. Mtaa wa Dosi
Diwani wa Kata hiyo ni Julian Bujugo.
HALI YA ELIMU.
Hali ya Elimu ni ya kawaida katika Kata hii, na inayo shule mbili za Msingi ambazo ni
• Ali Hassan Mwinyi.
• Liance Magomeni.
SEKONDARI.
Kata ya Magomeni haina shule ya Sekondari.
MAHUSIANO.
Mahusiano ya ofisi ya Kata na wananchi wake ni mazuri.
HALI YA AFYA.
Hali ya Afya ni nzuri katika Kata hii ya Magomeni, kwani hakuna mlipuko wa magonjwa ya aina yoyote.
MIRADI YA KUJIVUNIA.
Taasisi ya kutoa mikopo kwa wananchi hasa wafanyabiashara wadogo wadogo wa maeneo mbalimbali.(Pride).
Dar es salaam, Tanzania
Postal Address: P.O.BOX 31902 ,2Morogoro Road
Namba za simu: +255 22 2170173
Namba ya simu :
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz