KATA YA KIJITONYAMA.
Kata ya Kijitonyama ilianza mwaka 2000, na Asili ya Jina lake ni mto ambao ulikua ukitumika kuoshea nyama baada ya kuchinjwa na mto huo ulikua umezungukwa na wanyama mbalimbali na hapo ndipo lilipotokea jina la KIJITO CHA WANYAMA na hatimae KIJITONYAMA.
IDADI YA MITAA
Kata inajumla ya Mitaa nane kama ifuatavyo:-
1. Mtaa wa Mpakani A
2. Mtaa wa Mpakani B
3. Mtaa wa Alimaua A
4. Mtaa wa Alimaua B
5. Mtaa wa Kijitonyama
6. Mtaa wa Mwenge
7. Mtaa wa Nzasa.
8. Mtaa wa Bwawani.
Diwani wa Kata hii anaitwa Juma UloleUlole.
HALI YA ELIMU.
Kata inajumla ya shule tano za Msingi na moja ya Sekondari ambazo zote ni za Serikali, na kiwango cha ufaulu wa wanafunzi katika shule zote hizo ni cha kuridhisha.
HALI YA AFYA.
Kata inajumla ya zahanati mbili za Serikali ambazo hutoa huduma kwa wakazi wa Mitaa yote Nane.Kwa Ujumla hali ya Afya hasa upatikanaji wa Huduma za Afya ni mzuri, kwani pamoja na vituo hivyo viwili bado Kata iko jirani kabisa na Hospital ya Sinza Palestina pamoja na Hospitali ya Mwananyamala ambapo wananchi wanaweza kuonana na madaktari bingwa na kupatiwa huduma wanayostahili.
MIUNDOMBINU YA BARABARA NA MIFEREJI.
80% ya barabara za Kata ya Kijitonyama ni za vumbi.
HALIYA USAFI WA MAZINGIRA.
Kata inao utaratibu mzuri wa kudhibiti taka ngumu zinazozalishwa majumbani pamoja na maeneo ya biashara, ambapo Katika Kila mtaa Kunamkandarasi anaezoa taka na kuzifikisha dampo.
MAHUSIANO NA WADAU MBALIMBALI.
Wakazi wa Kijitonyama kwa ujumla wao wamekuwa wakitoa ushirikiano mkubwa katika kuchangia shughuli mbalimbali za maendeleo.
HALI YA MAENDELEO YA WATU NA MAKAZI.
Hali ya maendeleo ya watu na makazi ni nzuri, na hii imechangiwa na kuwepo na makampuni pamoja na taasisi, hali iliyoongeza mwingiliano wa watu na biashara kukua zaidi.
Dar es salaam, Tanzania
Postal Address: P.O.BOX 31902 ,2Morogoro Road
Namba za simu: +255 22 2170173
Namba ya simu :
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz