Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni inatekeleza program ya mfuko wa mikopo kwa wanawake na Vijana kama ilivyo kwa Halmashauri zote Nchini kufuatia agizo la Serikali la mwaka 1998 kuwa Halmashauri zote nchini zianzishe mfuko huo kwa kutenga asilimia 10% ya mapato yake ya ndani.
Halmashauri imekuwa ikifuata mwangozo wa mikopo kwa kuhakikisha inaboresha mfumo huo bila kukiukwa ili kuimarisha umiliki wa fedha za mfuko wa Halmashauri.
.LENGO LA KUBORESHA MFUMO.
• Kuimarishaumiliki wa fursa ya mikopo ya Manispaa.
• Kuondoa mgongano wa mikopo kati ya Manispaa na wakala.
• Kuimarishautambulisho wa walengwa kwa kuzingatia mwongozo.
• Kuondoa gharama/udhamini wa wakala (10%) ya fedha za mikopo.
Kuanzia mwaka huu wa fedha 2017/2018 utaratibu wa utoaji wa mikopo utakuwa kama ifuatavyo:-
Mchakato wote wa utoaji wa Mikopo utasimamiwa na kuratibiwa na Halmashauri kupitia idara ya Maendeleo ya Jamii, kuanzia uhamasishaji wa mikopo, kuainisha vikundi hadi hatua ya vikundi kupata mikopo yao na kufanya marejesho
MCHAKATO WA UKOPESHAJI.
• Uhamasishaji
• Uainishaji wa vikundi
• Majukumu ya wadau/viongozi
• Kujenga uwezo wa vikundi
• Ukopeshaji
• Urejeshaji
• Usimamizi na ufuatiliaji.
UHAMASISHAJI.
• Viongozi wa ngazi mbalimbali za uongozi watafanya uhamasishaji juu ya mikopo ya masharti nafuu kwa wanawake na vijana.
• Baada ya Uhamasishaji , wananchi wataelekezwa kwenda kwa Afisa Maendeleo ya Jamii wa Kata husika ili kuendelea na hatua zinazofuata.
• Pia utafanyika uhamasishaji wa uundaji wa vikundi na kuvijengea uwezo ili kuwa na sifa .
Baada ya uhamasishaji na uundwaji wa vikundi, zoezi litakalofuata ni kuvitambua vikundi ambavyo vitakuwa na sifa ya kukopesheka kwa kufanya yafuatayo:-
• Vikundi vya wakopaji watajiorodhesha katika ofisi zaoza Kata kwa Afisa Maendeleo ya Jamii.
• Kuainisha nakuchambua vikundi vinavyostahili kupewa mikopo.
• Kutoa hati ya usajili kwavikundi.
UNITI YA USIMAMIZI.
Katika ngazi ya Manispaa,kutakuwa na unit ya Mikopoambayo itakuwa na:-
1. Afisa Maendeleo ya Jamii-Mratibu
2. Mhasibu
3. Mwanansheria
4. Mchumi.
MAJUKUMU YA WADAU /VIONGOZI WA KATA
• Viongozikatika ngazi na kada mbalimbali watafanya uhamasishaji kwa ajiliya wananchi kutambua fursa ya mikopo.
• Ofisi ya Mtaaitahusikana kuwatambulishawakopajikuthibitishaukaaziwao katika mitaa yao.
• Wajumbe waKamati ya Maendeleo ya Kata watahusika nakupitishamajina na vikundivinavyostahilikupatiwa mikopo.
• Afisa Maendeleo ya Jamii atahusika na uratibuwa zoezila kuainisha vikundi vinavyostahili kupata mikopo, kujenga uwezo wa vikundi,nakuviwasilihaofisi uratibu wa Mikopo.
MAMBO YA KUZINGATIA
• UmriwaMkopaji-Kuanzia miaka 18.
• Wanaume iwe ni kati ya miaka 18hadi 35
• Shughuli ambazo zitapewa kipaumbele ni pamoja na viwanda vidogo vidogo na vikundi vyenye wananchama wenye ulemavu/vikundi vya wenye ulemavu.
• Wakopaji kuwa na utambulisho wa makazi kwa kuwasilisha barua ya Mtendaji wa Mtaa anakotokea.
• Vikundi kuwa na Katiba.
• Kusaini mkataba ulioambatishwa majina ya wanakikundiikionesha malengo ya mkopo ya kilamwanakikundikwa kila awamu ya mkopo anaoomba.
KUJENGA UWEZO WA VIKUNDI.
• Kila kikundi kitalazimika kufungua Akaunti katika Benki itakayokubaliwa.
• Vikundivitakavyokuwa na sifa ya kukopeshwa vitapatiwa mafunzo juu ya uwekaji wa akiba, kuandaakatiba,ukopaji naurejeshaji wa mikopo.
• Afisa Maendeleo ya Jamii atawasilisha taarifa ya vikundikwenye kamati ya maendeleo ya kata kwa ajili ya uchambuzi wa hatua ya awali.
UKOPESHAJI.
• Kila mwanakikundi ataainisha kiasi cha Mkopo anachohitaji na muda wa marejesho.
• Mikopo ya wanakikundi itajumlishwa na kupata kiasi cha mkopo wa kikundi.
• Kutokana na mahitaji ya kila mwanakikundi, itapigwa hesabuya rjrsho kwa wiki.
• Kila kikundi kitaingiziwa fedha katika akaunti katika Benki itakayokubaliwa.
UREJESHAJI WA MIKOPO.
• Kilamwanakikundi atarejesha kiasi cha rejesho lake kwa mkusanyaji wa fedha wa kikundi.
• Fedha zikishakusanywa ,mkusanya fedha atapeleka marejesho kwenye akaunti maalum ya Manispaa.
• Mkusanya fedha atawasilisha passbookpamoja na pay slip kwa Afisa Maendeleo ya Jamii wa Kata Husika.
NB:Kila kikundi kitalazimika kusaini mkataba wa kumdhamini mwanakikundi mwenzao na kuhakikisha wanabeba deni la mwanakikundi mwenzao pindi anaposhindwakulipa deni lake.
USIMAMIZI NA UFUATILIAJI.
• Mfumo wa marejesho utatumika kwa kushirikianana Maafisa waBenki kupitia vituovitakavyoainishwa na Kata.
• Kata itakayofanya vizuri kwa wakopaji wake kurejesha mikopo kwa zaidi ya asilimia 95% (95%)itaongezewa kiwango cha fedha za Mikopo.
• Kata ambazo hazitafanya vizurri hazitaongezewa fedha nyingine kwa mwaka unaofuata hadi marejesho ya fedha za awali yafikiezaidi ya asilimia tisini na tano(95%).
• Kila mwisho wa mwaka wa fedha itafanyika tathmini yakuzitambua Kata ambazo zimefanya vizuri na zile ambazo hazikufanya vizuri.
• Taarifa ya Mikopo itatolewa katika taarifa ya utekelezaji wa miradi kila robo ya mwaka katika Baraza la Madiwani.
MASWALA YA KUZINGATIA.
• Kushirikiana naBenki itakayopendekezwa kwa ajili ya kurahisisha ufuatiliaji wamarejesho.
• Benki zinazopendekezwa ni TWB,NMB,CRDB, TPB, na DCB kwani Benki hizini za Serikali na pia zina huduma kwa ajili ya vikundi.
UPATIKANAJI WA FEDHA.
• Inapendekezwa kuwa mikopo itolewe mara 4 kwa mwaka (mara moja kwa kila robo ya mwaka).
• Fedha zilizokusanywa na kuchangiwa kwenye mfuko zitatolewa kwa kuzingatia uwiano kwa Kata.
Dar es salaam, Tanzania
Postal Address: P.O.BOX 31902 ,2Morogoro Road
Namba za simu: +255 22 2170173
Namba ya simu :
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz