KATA YA BUNJU.
Kata ya Bunju ni miongoni mwa Kata kongwe ndani ya Manispaa ya Kinondoni. Jengo la ofisi ya Kata hii lilizinduliwa tarehe 29/06/2001 na kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa wa Mwaka huo ambaye ni Ndg Fatma Juma Shomari.
IDADI YA MITAA.
Kata ya Bunju inajumla ya Mitaa sita kama ifuatavyo:-
1. Mtaa waBasihaya.
2. Mtaa wa Boko,
3. Mtaa wa Dovya
4. Mtaa wa Kilungule
5. Mtaa wa Mkoani
6. Mtaa wa Bunju A.
Diwani wa Kata hii ya Bunju ni Kheri Nassor Missinga.
HALI YA ELIMU.
Hali ya Elimu katika Kata ni ya kuridhisha na wanafunzi wake hujitahidi kufikia lengo la ufaulu kwa asilimia zinazotakiwa. Kata hii inazo shule za Msingi na Sekondari ambazo ni za Serikali.
SHULE ZA MSINGI ZA SERIKALI.
Kata ya Bunju inazo shule nne za Msingi za Serikali kama zifuatazo:-
• Shule ya Msingi Boko.
• Shule ya Msingi Mtambani
• Shule ya Msingi Boko NHC
• Shule ya Msingi Bunju A.
SHULE ZA SEKONDARI ZA SERIKALI.
Kata hii ya Bunju inazo pia shule mbili za Sekondari za Serikali kama ifuatavyo:-
• Shule ya Sekondari Boko
• Shule ya Sekondari Bunju.
HALI YA AFYA.
Hali ya Afya ya Kata ya Bunju ni ya Kuridhisha. Kata hii inazo zahanati mbili ambazo ni:-
• Boko Dispensary inayohudumia wakazi wa Mtaa wa Boko, Basihaya na maeneo ya Jirani.
• Bunju Dispensary inayohudumia maeneo yote yanayozunguka Bunju na Vitongoji vyake.
HALI YA MIUNDOMBINU YA BARABARA NA MIFEREJI.
Kata ya Bunju inazungukwa na barabara za lami nne ambazo ni Barabara ya Boko chama, kwenda ununio na kutokea Kunduchi ambayo pia inamifereji ya maji ya maji ya mvua, pia kuna barabara ya njia ya panda mbweni- Kwenda malindi Mbweni na ambayo pia inamifereji na barabara nyingine kuanzia kilungule kwenda Mbweni . Lakini pia Kata ya Bunju inapitiwa na barabara kubwa ya Bagamoyo kwa Mitaa yote sita.
HALI YA USAFI NA MAZINGIRA.
Hali ya usafi wa Kata ya Bunju ni wa kuridhisha, kwani Mitaa yote sita inayo wakandarasi wanaozoa taka na kusafirisha kwenda kutupa.
MAHUSIANO NA WADAU.
Katika Kata ya Bunju, mdau Mkubwa wa Maendeleo ni kiwanda cha Cement cha Wazo ambacho mara kadhaa kimekuwa kikisaidia maendeleo katika Mitaa ya Basihaya na Boko hasa katika kusaidia vifusi vya barabara , vyandarua na Mazingira. Wapo pia wadau wadogo wadogo wanaosaidia katika Kata.
MIRADI YA KUJIVUNIA.
Kata ya Bunju inajivunia hasa katika miradi ya Elimu kwani pamoja na kuwa na shule nne za Msingi na Shule mbili za Sekondari bado imeanzisha ujenzi mpya wa shule ya Msingi katika Mtaa wa Mkoani.
HALI YA MAENDELEO YA WATU NA MAKAZI.
Hali ya maendeleo ya watu na makazi inakua kwa Kasi kwa kuwa watu wengi wamejenga nyumba za Kisasa hasa katika eneo la mradi wa viwanja 2000(Bunju Beach),na eneo la Boko beach ambako kuna miundombinu yote ya mipangomiji.
Pia katika maeneo yasiyopimwa ujenzi unafanyika kwa kasi.
Dar es salaam, Tanzania
Postal Address: P.O.BOX 31902 ,2Morogoro Road
Namba za simu: +255 22 2170173
Namba ya simu :
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz