Kuelekea miaka 60 ya Uhuru yenye kauli mbiu isemayo "Miaka 60 ya Uhuru, Tanzania imara kazi iendelee" Manispaa ya Kinondoni imeunga Serikali mkono kwa kufanya maonesho ya biashara ya wajasiriamali .
Akizindua maonesho hayo kwa niaba ya Katibu Tawala wa Wilaya, Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Ndugu John Deogratius amesema wajasiriamali hawa ni wale waliowezeshwa mkopo wa asilimia kumi kwa lengo la kuwawezesha kujikwamua kiuchumi.
Ameongeza kuwa Watanzania wanatakiwa kuwa wazalendo kwa kupenda na kujali vya Watanzania kwa kuwaunga mkono wajasiriamali wetu ili kwa pamoja tuweze kukusa soko la bidhaa za ndani.
Maonesho haya yamefanyika eneo la viwanda Mwananyamala ambapo wajasiriamali wafanyabiashara wameonesha bidhaa zao walizozitengeneza kwa mikono na nguvu zao.
Imeandaliwa na
Kitengo Cha Habari na Uhusiano.
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.