Kata ya Kunduchi ilianzishwa mwaka 1970 na uchaguzi wa kwanza wa viongozi wa vijiji ulifanyika mwaka 1971. Eneo la Kata ya Kunduchi wakati wa ukoloni lilijulikana kwa jina la MAWENI eneo ambalo kwa kipindi hicho au mpaka sasa lina machimbo ya kokoto na mawe.
Maana ya neno Kunduchi MAKALIO KUWA WAZI kutokana na wakazi wake kuwa na mazoea ya kuvaa nguo nusu ili zisilowe walipokuwa wanavuka maji ya bahari kuelekea mtumbwini. Neno hili ni la Kizaramo.
Kata ya Kunduchi ina jumla ya mitaa sita (06) ya Kiserikali ambayo ni: -
Hali ya elimu katika Kata ya Kunduchi ni ya kuridhisha, hasa elimu ya awali, msingi, sekondari na uwepo wa chuo cha elimu ya juu.
Kata ya Kunduchi inazo shule za msingi saba (07) za serikali kama ifuatavyo: -
Kata ya Kunduchi ina shule za awali za binafsi kumi (10) kama ifuatavyo: -
Kata ya Kunduchi inazo shule za msingi kumi (10) za binafsi kama ifuatavyo: -
Kata ya Kunduchi inazo shule mbili (02) za sekondari za serikali kama ifuatavyo: -
Kata ya Kunduchi inazo shule tano (05) za sekondari za binafsi kama ifuatavyo: -
Kata ya Kunduchi ina Chuo Kikuu kimoja cha serikali kinachojulikana kwa jina la Chuo Kikuu Mzumbe.
Hali ya Afya katika Kata ya Kunduchi ni ya kuridhisha kwani ina Hospitali, Kituo cha Afya na Zahanati za serikali na binafsi.
Kata ya Kunduchi ina Kituo cha Afya kimoja cha binafsi kinachoitwa Tegeta Mission.
Kata ya Kunduchi ina Zahanati tatu (03) za serikali kama ifuatavyo: -
Kata ya Kunduchi ina Zahanati saba (07) za binafsi kama ifuatavyo: -
Hali ya miundombinu ya barabara katika Kata ya Kunduchi ni ya kuridhisha. Mtandao wa barabara za lami katika Kata ni barabara ya Tegeta Nyuki - Kondo, Kilongwima, Kunduchi beach, Ras Kilomoni.
Mahusiano ya wadau wa maendeleo na uongozi wa Kata na mitaa ni mazuri. Kata inashirikiana na wadau mbalimbali katika kufanikisha shughuli zake. Wadau hao ni pamoja na Rottery Club, Massana hospitali, Water aid.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.