Kata ya Mbweni ni miongoni mwa Kata 20 za Manispaa ya Kinondoni. Asili ya jina Mbweni ni uwepo wa bandari kubwa ya asili iliyokuwa inatumika na Wareno enzi za ukoloni, jina ambalo wageni na wenyeji walilitumia wakimaanisha ni sehemu tulivu.
Sehemu ya BANDA MOJA, kwa sasa ni MITI 3 kulikuwa na makaburi ya Wahindi, Waarabu na Wasomali ambao wote walifika katika vipindi tofauti eneo la Mbweni kwa ajili ya kupakia na kushusha bidhaa zao kwa kutumia eneo la bandari lilikokuwa likijulikana kwa jina la STAHABUU ambalo kwa sasa kuna kambi ya kijeshi ya 19 (JKT). Uwepo wa bandari hii ulipelekea mji kutanuka haswa maeneo ya Mpiji na Teta.
Mtaa wa Teta ulikuwa na mashamba ya miembe, minazi na mikorosho. Bidhaa mbalimbali zilikuwa zinasafirishwa katika eneo hili zikiwemo vipusa na mchele kwenda Uarabuni kwa kutumia majahazi makubwa.
Eneo ambalo kwa sasa ni Mtaa wa Maputo kulikuwa na shamba enzi za ukoloni na Bagamoyo ilikuwa ni Makao Makuu. Kiongozi mkuu wa eneo hili alkuwa akifahamika kwa jina la GULAMRASSUR na alikuwa ni LALIWI, cheo kama cha Mkuu wa Wilaya (DC) kwa sasa. Kazi yake kubwa ilikuwa ni kusimamia mashamba na wakulima ambao walilazimishwa kulima mazao ya korosho na mihogo.
Mtaa wa Malindi Estate paliitwa MMARANII na palikuwa na jela ya watoto na msikiti ambao ulijengwa na mzungu aliyeitwa BELL ambapo kwa sasa ndio eneo la USALAMA WA TAIFA.
Kata ya Mbweni inayo mitaa mitano (05) ambayo ni: -
Hali ya elimu katika Kata ni ya kuridhisha, hasa elimu ya msingi na sekondari pamoja na uwepo wa chuo. Aidha kuna shule sita ambazo ni: -
Kata ya Mbweni inazo shule sita (06) za sekondari za serikali na binafsi ambazo ni: -
Katika Kata ya Mbweni kuna Chuo cha Afya kinachojulikana kwa jina la Nyaishozi College of Health.
Hali ya Afya katika Kata ya Mbwenii ni ya kuridhisha kwani ina Hospitali ya binafsi ijulikanayo kwa jina la Hospitali ya St. Joseph na Zahanati ya serikali ijulikanayo kwa jina la Zahanati ya Mbweni.
Mahusiano na wadau wa maendeleo ni ya wastani maana hakuna makampuni binafsi katika Kata.
Katika Kata ya Mbweni, mipangomiji na uwepo wa miundombinu ya huduma mbalimbali ni ya kuridhisha.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.