Kijiji cha Makumbusho kilichopo pembezoni ya barabara ya Ally Hassan Mwinyi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kilianzishwa mwaka 1996 kwa lengo la kuhifadhi na kuonyesha tamaduni mbalimbali za makabila ya Kitanzania.
Kijiji cha Makumbusho ni kivutio kizuri cha utalii kinachoonesha tamaduni za makabila yasipungua 100 ya Tanzania. Kinazo nyumba za asili zilizojengwa kwa tope na kuezekwa kwa nyasi na tope. Vivevile kina michoro ya asili, mikeka iliyosukwa kwa mikono na ngoma za asili zinazovutia kucheza.
Makumbusho haya yamehifadhi na kuonyesha namna yalivyo makazi mbalimbali ya Watanzania kote nchini na pia hutoa fursa kwa wageni kusikiliza ngoma za asili kutoka makabila tofauti tofauti.
Kutembelea Kijiji cha Makumbusho ni sawa na kuitembelea Tanzania nzima ndani ya muda mfupi, kwa kuweza kuona na kujifunza juu ya tamaduni za makabila mbalimbali yaliyopo Tanzania.
Wageni na wenyeji pia wanapata fursa ya kula vyakula mbalimbali vya asili na kuburudika na ladha yake murua, pamoja na wasaa wa kufanya manunuzi ya bidhaa tofauti tofauti za kiutamaduni.
Nyumba za asili katika Kijiji cha Makumbusho
Mahali pekee pa kuona kazi za wasanii na kugundua vipaji vyao vya kipekee katika sanaa za kitamaduni ni katika Nyumba ya Sanaa inayopatikana katika mtaa wa Ohio karibu na Hoteli ya Movenpick.
Maonyesho ya nyimbo za kitamaduni huchezwa kila Ijumaa. Ngoma na nyimbo za asili huchezwa kwa ala za muziki kutoka kwa vikundi vya Simba Theatre International, Super Kamambe na Sisi Tambala.
Kituo hiki kinakaribisha wenyeji na wageni mbalimbali kujionea na kuburudika kwa kazi za wasanii na urithi wa kitamaduni wa Jiji la Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla.
Nyumba ya Sanaa
Pembezoni tu mwa Jiji, katika barabara ya kuelekea Bagamoyo, mwendo wa takribani dakika 45 kutoka katikati ya Jiji, kuna Soko la Wachongaji vinyago cha Mwenge maarufu kama Mwenge vinyago ambalo lilianzishwa mnamo mwaka 1984. Vinyago hivi vinavyochongwa vizuri kabisa vinakuwa katika muonekano na ukubwa tofauti tofauti.
Kituo cha Wachongaji vinyago Mwenge kimekua na wanachama wa chama cha wachongaji vinyago wa Tanzania. Mwenge vinyago ina soko linalojumuisha maduka madogo na fremu zinazoonyesha na kuuza sio tu vinyago lakini pia nguo za kitamaduni, kanga, vikoni na picha za tinga tinga. Vinyago vinachongwa kwa kutumia mti wa Mpingo, Mkangazi na Mwarobaini.
Katika Mwenge Vinyago kuna jamii kubwa ya wachongaji vinyago na wachoraji wakiwa sura za bashasha wakitekeleza majukumu yao kwa bidii na ufanisi mkubwa.
Wageni mbalimbali wanapata fursa ya kujionea namna vinyago vinavyotengenezwa ikiwa ni pamoja na kuzungumza na wasani hao kuhusu maisha yao na mazingira kwa ujumla.
Kwa manunuzi yote ya vinyago na picha za rangi za kuvutia. Mwenge vinyago ndiyo suluhisho.
Hivi pia ni maarufu sana Tanzania, ni mtindo wa kupaka rangi wa Tingatinga. Mtindo huu ambao hutokana na kutumia rangi za mafuta na kutengeneza michoro ya katuni, huvutia sana. Usiondoke Dar es Salaam kabla haujanunua Tingatinga na uweke kwenye fremu ufikapo nyumbani. Utapata aina nyingi katika Kituo cha sanaa Tingatinga.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.