Kata ya Wazo ni Kata ambayo ilizaliwa na Kata ya Kunduchi. Kwa kipindi hicho Kata ya Kunduchi ilikuwa inaundwa na mitaa sita (06) ambayo ni Tegeta, Wazo Madale, Mtongani, Ununio na Salasala.
Mnamo mwaka 2009 Kata ya Kunduchi ikagawanyika na kuzaliwa Kata ya Wazo.
Jina la Wazo lilitokana na uwepo wa kiwanda cha saruji (WAZO HILL -TWIGA CEMENT) na watu wengi walikuwa wakifanya kazi katika kiwanda hicho na hapo ndipo jina la Wazo likazaliwa. Kwa kipindi hicho Kata ya Wazo ilikuwa inaundwa na Mitaa sita ambayo ni Salasala, Wazo, Madale, Mivumoni, Kilimahewa na Kisanga. Ilipofika mwaka 2014 Kata ya Wazo iliongezewa mitaa miwili ambayo ni Nyakasangwe na Kilimahewa juu.
ASILI YA WATU WA WAZO; Kabla ya mgawanyiko wa Kata ya Kunduchi na Wazo asilimia kubwa ya eneo la Wazo lilikuwa ni mashamba na mapori na wenyeji wengi walikuwa ni wakulima na wafugaji. Wafanyakazi wachache ni waliokuwa wakifanya kazi kiwanda cha saruji cha Twiga pamoja na wavuvi. Kuna mchanganyiko wa makabila mbalimbali ndani ya Kata ya Wazo ikiwemo, Wamakonde, Wazaramo, Wangoni, Wahehe, Wamwera n.k.
ASILI YA JINA LA MTAA MADALE; zamani Madale ilikuwa ikijulikana kama Madala kwa lugha ya King’indo ikimaanisha kuwa ni sehemu iliyokuwa na tabu, pagumu kuishi. Miaka ya 1980/1990 kulikuwepo na kambi ya SCOUT iliyoanzishwa na Marehemu Hayati Rashid Mfume Kawawa. Bahati mbaya wafadhili waliokuwa wanawafadhili vijana wa kambi hiyo wazungu kutoka Norway walikuwa wanashindwa kutamka neno Madala badala yake wakawa wanatamka Madale. Kwa hiyo majina yote mawili yakaendelea kutumika mpaka mwaka 2014 jina la Madala likafa na Kiserikali likabaki Madale.
Kata ya Wazo ina jumla ya Mitaa nane (08) kama ifuatavyo:-
1. Mtaa wa Salasala
2. Mtaa wa Kilimahewa
3. Mtaa wa Kilimahewa Juu
4. Mtaa wa Wazo
5. Mtaa wa Kisanga
6. Mtaa wa Mivumoni
7. Mtaa wa Madale
8. Mtaa wa Nyakasangwe
Hali ya elimu katika Kata ya Wazo ni ya wastani.
Kata ya Wazo inazo shule tano (05) za msingi za serikali ambazo ni :-
Kata pia ina shule za awali na msingi za binafsi 15.
Kadhalika Kata ya Wazo inazo pia shule tatu (03) za sekondari ambazo ni za Serikali kama ifuatavyo:-
Kata pia ina shule za sekondari za binafsi 14.
Kata ya Wazo ina chuo kimoja cha serikali ambacho ni KMC Vocational Training Centre kilichopo mtaa wa Mivumoni pamoja na chuo binafsi cha Amazon College.
Hali ya Afya katika Kata ya Wazo ni ya kuridhisha kwani ina Zahanati na Vituo vya Afya vya serikali na binafsi.
Vituo vya Afya vilivyopo ni viwili (02) ambavyo ni vya binafsi kama ifuatavyo: -
Zahanati zilizopo katika Kata ya Wazo ni saba (07) ambazo tatu (03) kati ya idadi tajwa ni za serikali na nne (04) ni za binafsi kama ifuatavyo: -
Kata ya Wazo inayo miundombinu ya barabara za lami na changarawe kuu nne ambazo ni;
Kata ya Wazo pamoja na wananchi wake inayo mahusiano ya kuridhisha na wadau wake, na ndio maana wanashirikiana kwa pamoja katika kusukuma maendeleo ya Kata yao.
MIRADI YA KUJIVUNIA KATIKA KATA
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.