Kata ya Makumbusho ilianzishwa mwaka 1999 bada ya kugawanywa kwa Kata ya Mwananyamala. Asili ya jina hili ni kijiji cha Makumbusho ambapo palikuwa na kituo cha basi kilichoitwa Makumbusho.
Kata ya Makumbusho ni moja Kata zinazounda Halmshauri ya Manispaa ya Kinondoni, aidha Kata hii imepakana na Kata ya Kijitonyama upande wa Kasikazini, Kusini imepakana na Kata ya Ndugumbi, Mashariki imepakana na Kata ya Mwananyamala na Magharibi imepakana na Kata ya Tandale.
Idadi ya Watu
Kwa mjibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022, Kata ya Makumbusho ina jumla ya Watu 52347 kati ya hao Wanaume wapo 25876 na Wanawake ni 26471.
Idadi ya Mitaa
Kata ya Makumbusho Ina jumla ya Mitaa Sita ambayo ni;
1 Mtaa wa Minazini
2 Mtaa wa Makumbusho
3 Mtaa wa Mchangani
Kata ya Makumbusho imepitiwa na Barabara kuu Mbili ambazo ni Barabara ya Mwananyamala na Barabara ya Mwinyijuma, Mbali na Barabara hizo kuu mbili pia Kata ya Makumbusho ina jumla ya Barabara 28 katika Mitaa yote Sita, kati ya hizo 2 za kiwango cha lami, 1 ya zege na 25 ni za vumbi.
Biashara na Uwekezaji
Kata ya Makumbusho ina Jumla ya Masoko 2. Ambayo ni Soko la Mfavesco na Soko la Kisiwani, pia Wananchi na Wakazi wa Kata ya Makumbusho wanajishughulisha na Biashara ndogo ndogo, Kilimo mjini na Ajira.
Hali ya Elimu katika Kata
Kata ya Makumbusho ina jumla ya Shule Saba ambazo zote zinamilikiwa na Serikali, kati ya hizo Sita ni za Msingi na Moja ya Sekondari.
Shule za Msingi
Jina la Shule
|
Wanafunzi
|
Jumla
|
Walimu
|
Jumla
|
||||
Makumbusho S/m
|
Me
|
Ke
|
767
|
Me
|
Ke
|
20
|
||
404
|
363
|
4
|
16
|
|||||
Victoria S/m
|
Me
|
Ke
|
697
|
Me
|
Ke
|
13
|
||
343
|
353
|
2
|
11
|
|||||
Mwananyamala S/m
|
Me
|
Ke
|
587
|
Me
|
Ke
|
15
|
||
318
|
269
|
3
|
12
|
|||||
Minazini S/m
|
Me
|
Ke
|
845
|
Me
|
Ke
|
14
|
||
439
|
406
|
1
|
13
|
|||||
Mwananyamala Kisiwani
|
Me
|
Ke
|
1420
|
Me
|
Ke
|
22
|
Mchangani S/m
|
Me
|
Ke
|
1526
|
Me
|
Ke
|
28
|
740
|
789
|
4
|
24
|
Hali ya Afya katika Kata
Kata ya Makumbusho ina jumla ya Zahanati Nne ambapo 3 ni Sekta Binafsi na 1 ni Serikali. Pia kuna Kituo Kimoja cha Afya ambacho ni Sekta Binafsi, hakuna Hosptali yoyote.
S/n
|
Jina
|
Hadhi
|
Umiliki
|
1
|
KAM Mwananyamala
|
Zahanati
|
Binafsi
|
2
|
Kisiwani
|
Zahanati
|
Binafsi
|
3
|
Makumbusho
|
Zahanati
|
Serikali
|
4
|
Minazini
|
Zahanati
|
Binafsi
|
5
|
Sisa
|
Kituo cha Afya
|
Binafsi
|
Maendeleo ya Jamii
Mahusiano na Ushirikiano na Wadau wa Maendeleo
Kata ya Makumbusho inashirikiana vema na Wadau wa Maendeleo katika kuhakikisha gurudumu la Maendeleo linasonga mbele, ambapo Wadau wanaoshirikiana nao ni wafanyabiashara ndogo ndogo.
Hali ya Ulinzi na Usalama.
Hali ya ulinzi na usalama katika Kata ya Makumbusho inaridhisha kwani amani imetawala kutokana na uwepo wa vituo Viwili vya Polisi ambavyo ni; Kituo cha Polisi cha Mwinjuma na Kituo cha Polisi cha Minazini. Pamoja na uwepo wa Vituo hivyo vya Polisi kila Kata ina kikundi cha ulinzi shirikishi ambao wanashirikiana bega kwa bega na Askari Polisi kuhakikisha ulinzi unakuwa imara siku zote.
Maafisa Ngazi ya Kata
Mtendaji Kata 1
Watendaji wa Mitaa 6
Afisa Ustawi wa Jamii 1
Afisa Elimu Kata 1
Afisa Kilimo na Mifugo 1
Afisa Afya 2
Miradi ya Maendeleo
Shule ya Msingi Mchangani
Shule ya Msingi Makumbusho
Kata ya Makumbusho ina jumla ya sita (6) mitano ya Kiserikali ambayo ni: -
Mahusiano ya wadau wa maendeleo na uongozi wa Kata na Mitaa ni mzuri, ikiwemo kampuni ya ulinzi ambayo Kata inashirikiano nayo katika masuala ya maendeleo.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.