Kata ya Tandale iko katika Tarafa ya Kinondoni, jimbo la Kinondoni Manispaa ya Kinondoni, imepakana na Manispaa ya Ubungo kwa upande wa Magharibi. Kihistoria asili ya jina hili linatokana na bwawa la maji la Tandale na ilianzishwa mwaka 1995.
Kata ya Mzimuni ina jumla ya mitaa sita (06) ya Kiserikali ambayo ni: -
Hali ya elimu katika Kata ni ya kuridhisha, hasa elimu ya awali na msingi kwa uwepo wa shule za serikali na binafsi. Kata ya ya Tandale haina shule ya sekondari ya serikali , binafsi au taasisi.
Kata ya Tandale inazo shule za msingi nne (04) za serikali na shule za awali za binafsi thelathini (30)
Hali ya Afya katika Kata ya Tandale ni ya kuridhisha kwani ina Kituo cha Afya cha serikali na Zahanati za binafsi.
Kata ya Tandale ina Kituo cha Afya cha serikali kijulikanacho kwa jina la Kituo cha Afya cha Tandale.
Kata ya Tandale inazo Zahanati sita (06) za binafsi ambazo ni: -
Hali ya miundombinu ya barabara katika Kata ya Tandale ni mizuri na barabara zote ni za kiwango cha lami na zege na zimewekewa taa za barabarani.
Kata ya Tandale ina mahusiano mazuri na wadau wa maendeleo na ndio wamewezesha kujenga ofisi ya Serikali ya Mtaa katika mtaa wa Sokoni. Pia Kata ya Tandale inapokea misaada mbalimbali ya kimaendeleo kutoka kwenye taasisi za umma, binafsi na jamii ya Tandale kwa ujumla.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.