Kata ya Magomeni ilianzishwa mwaka 1995 ikiwa na mitaa mitano. Mnamo mwaka 2000 Kata hii iligawanywa na kupatikana Kata ya Ndugumbi.
Asili ya jina Magomeni ni miti iliyokuwa inapatikana maeneo hayo, miti hiyo ilikuwa inatoa magome mengi na makubwa hivyo kupelekea eneo hili kuitwa MAGOMENI.
Kata ya Magomeni ina jumla ya mitaa mitano ya Kiserikali ambayo ni: -
Hali ya elimu katika Kata ni ya kuridhisha, hasa elimu ya awali, msingi na sekondari.
Kata ya Magomeni inazo shule mbili (2) za awali na msingi ambazo ni: -
Kata ya Magomeni ina shule moja ya sekondari ya serikali inayoitwa Magomeni sekondari.
Hali ya Afya katika Kata ya Magomeni ni ya kuridhisha kwani ina Zahanati za serikali na binafsi zijulikanazo kwa majina ya Zahanati ya Magomeni na Mchichani mtawaliwa.
Kata ya Magomeni ina mtandao wa barabara za kiwango cha lami zenye urefu wa kilomita 5.
Mahusiano ya wadau wa maendeleo na uongozi wa Kata na Mitaa ni mzuri, kwani wako mstari wa mbele kuchangia shughuli za kijamii na miradi ya maendeleo.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.