Kata ya Mzimuni ndio Kata kongwe ambayo ndiyo iliyobeba watu mashuhuri, waasisi wa Chama Tawala, na wapigania Uhuru waliopanga mikakati ya kuikomboa Tanganyika na kuwa huru. Mwalimu Nyerere alijenga nyumba na kuishi hapo ambapo kwa sasa ni Makumbusho ya Taifa.
Viongozi wengine wa kitaifa waliokuwa wakiishi hapo ni pamoja na: - Rashid Mfaume Kawawa, Abdul Kandoro, Ndugu Kambona, Sheikh Amri Abeid Kaluta, Mzee Songambele, Lucy Lameck, Chifu Abdallah Fundikira, Tewa said Tewa.
ASILI YA JINA LA MZIMUNI: - Jina la Mzimuni limetokana na uwepo na msitu na pori kubwa lenye wanyama wakali pamoja na nyoka wengi, na ndani ya eneo hilo kulikuwa na visima viwili vya chemchem. Kimoja kati ya visima hivyo kilikuwa kinatoa maji mengi ambayo watu walikuwa wakiyatuia kwa kunywa, kuoga (kuondosha mikosi/matatizo mbalimbali) mfano wenye ugonjwa na kwa matambiko ya kijadi.
Kisima hiko kilikuwa na maajabu wakati mwingine maji yake hua mekundu au meusi, na ikalazimika watu wasiende katika kisima hiko kati ya saa 6 hadi 8 mchana, na saa 12 jioni na kisima kingine maji yake yalikua yakitoka katikati ya mwembe mkubwa, na kilikuwa na nyoka mkubwa, ambapo watu na wanyama wakifika katika kisima hiko, walikua wakipotea.
Mmoja wa wazee marufu Bwana Ramadhani Madogoli, ndiye alikua akitumia sana eneo hilo kwa shughuli za matambiko, ikiwemo ngoma ya asili iitwayo Mganda. Pia kulikua na mwembe ng'ongo mkubwa na katikati ya shina la mwembe huo palikua na tundu la wazi ambapo wakati mwingine unaweza kukuta chakula au fedha.
Lakini pia palikuwa na makaburi ya asili ambayo nyakati za usiku kulikuwa na mambo ya ajabu. Na wakazi wa eneo hilo walikua wakisoma shule ya Mzizima, ndipo baadaye Wazungu wakataka kujenga hospitali, lakini wazee walikataa na kuomba wajengewe shule, na hatimaye eneo hilo likajengwa shule ya msingi na kuitwa Mzimuni ambayo ilikwepo kabla ya uhuru miaka ya 1954. Hospitali/Kituo cha Afya kikajengwa eneo la Magomeni na miongoni mwa watu maarufu waliosoma shule ya msingi Mzimuni ni: - Ramadhani Dau, Juma Kapuya, Saidi Mwambungu n.k
Madiwani wa kwanza waliongoza Kata hii ni pamoja na Mzee Luyaya, Mzee Chambuso, Ally Bwamkuu (2000) na Abdulkarim Mtoni (2000 – 2010).
Kata ya Mzimuni ina jumla ya mitaa minne (04) ya Kiserikali ambayo ni: -
Hali ya elimu katika Kata ni ya kuridhisha, hasa elimu ya awali, msingi na sekondari za serikali na binafsi.
Kata ya Mzimuni inazo shule za msingi mbili (02) za serikali kama ifuatavyo: -
SHULE ZA AWALI ZA NA MSINGI ZA BINAFSI:
Kata ya Mzimuni inazo shule za awali na msingi mbili (02) za binafsi kama ifuatavyo:-
Kata ya Mzimuni ina shule moja (01) ya sekondari ya serikali ijulikanayo kwa jina la Mzimuni sekondari.
Kata ya Mzimuni ina shule moja (01) ya sekondari ya serikali ijulikanayo kwa jina la Nur Islamic Seminari
Hali ya Afya katika Kata ya Mzimuni ni ya kuridhisha kwani ina Hospitali ya binafsi na Zahanati za serikali na binafsi.
Kata ya Mzimuni ina Hospitali moja (01) ya binafsi inayojulikana kwa jina la Hospitali ya Mikumi.
Zahanati zilizopo katika Kata ya Mzimuni ni nne (04) ambapo 1 kati ya idadi tajwa ni ya serikali inayojulikana kwa jina la Zahanati ya Mzimuni na za binafsi ni: Mosha dental clinic, Herbal clinic ya Wachina, na Omega dental clinic.
Hali ya miundombinu ya barabara katika Kata ya Mzimuni inaridhisha. Kata nzima ina barabara za kiwango cha lami zenye urefu wa kilomita 3.
Mahusiano na wadau wa maendeleo yapo vizuri, ambapo Kata inapata ushirikiano toka kwa wadau wafuatayo: - Benki ya NMB, TOTAL Petrol Station, HOTEL TRAVETINE, NORTHELAND HOTEL, BUTIAMA HOTEL, MIKUMI IN HOTEL, KISUMA BAR AND LODGE n.k
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.