i. Kuratibu na kusimamia uwepo wa miundombinu ya msingi toshelevu shuleni ikiwa ni ujenzi/ukarabati wa vyumba vya madarasa, vyoo vya wanafunzi, nyumba za walimu, maktaba, majengo ya utawala na vituo vya walimu.
ii. Kuhamasisha na kuratibu uandikishaji wa watoto wa rika lengwa katika darasa la awali, darasa la kwanza na MEMKWA ikiwa ni pamoja na wanafunzi wenye mahitaji maalum pamoja na kusimamia mahudhurio yao kwa shule za Awali na Msingi za Serikali na zisizo za Serikali.
iii. Kuratibu matumizi sahihi ya ruzuku za uendeshaji wa shule.
iv. Kuratibu na kusimamia utoaji wa elimu ya watu wazima na elimu nje ya mfumo rasmi kwa walioikosa katika vituo 18 vilivyosajiliwa.
v. Kufanya ufuatiliaji na kusimamia ufundishaji na ujifunzaji shuleni ili kuhakikisha ufaulu wa mtihani/upimaji wa kitaifa unaongezeka na hakuna mwanafunzi anayehitimu Elimu ya Msingi bila kumudu stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK).
vi. Kuratibu na kudhibiti uwepo wa vifaa toshelevu vya kufundishia na kujifunzia shuleni hususan vitabu vya kiada vinavyosambazwa na Serikali kupitia Taasisi ya Elimu Tanzania (TEA).
vii. Kuratibu zoezi la ukusanyaji na ujazaji wa takwimu za kielimu katika sensa ya elimu msingi.
viii.Kuthibitisha uhamisho wa wanafunzi wanaohama na kuhamia kutoka shule moja kwenda nyingine ndani na nje ya Manispaa.
ix. Kusajili madeni ya walimu yasiyo ya mshahara katika mfumo wa madeniMIS.
x. Kuendesha mafunzo ya mifumo ya FFARS, MadeniMIS, PReM na SiS pamoja na taratibu na kanuni za manunuzi ya umma kwa walimu wakuu wa shule za serikalii na zisizo za serikali ili kuwawezesha kutumia mifumo hiyo kwa ufanisi kwa utendaji kazi wa kila siku.
i. Kumshauri Mkurugenzi wa Halmashauri kuhusu shughuli zote zinazohusu Idara ya Elimu ya Sekondari
ii. Kusimamia mitihani yote ya ndani na ile ya Taifa yaani Mitihani ya kidato cha II, IV na VI.
iii. Kusimamia, kuratibu na kufuatilia shughuli za ujenzi wa miundombinu katika shule za Sekondari kama vile nyumba za walimu, madarasa, majengo ya utawala, maabara, maktaba na vyoo.
iv. Kusimamia na kuratibu shughuli zote za ukusanyaji, uchambuzi na kutafsiri takwimu za Idara ya elimu sekondari na kuzituma kwa wadau wa elimu
v. Kusimamia na kuratibu shughuli za uandaaji wa taarifa na kuzituma kwa wadau mbalimbali wa elimu ngazi ya Wilaya, Mkoa na Taifa
vi. Kusimamia na kuhakikisha kuwa wanafunzi wanapata taaluma kwa kiwango kilicho bora kwa mujibu wa Sera ya Elimu ya mwaka 1995 na 2014.
vii. Kusimamia na kuhakikisha nidhamu ya wanafunzi, walimu na watumishi wasio walimu inadumishwa shuleni
viii. Kusimamia na kuhakikisha fedha za Idara ya Elimu Sekondari zinatumika kwa kufuata kanuni, sheria, taratibu na miongozo ya fedha za Serekali za Mitaa
ix. Kuhakikisha vifaa vya kufundishia na kujifunzia vinapatikana katika shule za sekondari
x. Kuhakikisha kuwa shule zote za Sekondari zina samani za kutosha kwa ajili ya walimu na wanafunzi
xi. Kuandaa ajenda na kuhudhuria vikao vyote vinavyohusu Idara ya Elimu Sekondari
xii. Kuandaa taarifa za utekelezaji za Idara ya elimu sekondari za robo na mwaka na kuziwasilisha kwa wadau mbalimbali wa maendeleo kama vile Waheshimiwa Madiwani, Mkoa na Taifa
xiii. Kuandaa makisio ya bajeti ya Idara ya Elimu ya Sekondari kila mwaka.
xiv. Kupokea na kuwapangia vituo walimu na wafanyakazi wa idara wanaohamia au wanaoajiriwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.