Mji wa Kawe ulianza tangu miaka ya 1908. Kipindi hicho mji ulikuwa hapo lilipo eneo la Makaburi ya Mzimuni (Mwai Kibaki road). Asili ya jina la Kawe lilitokana na mwanamke mmoja aliyeishi maeneo hayo aliyeitwa Bi. Mwakawi. Bi. Mwakawi alipokufa alizikwa katika makaburi ya Mzimuni ambapo mbuyu mkubwa ulioota juu ya kaburi lake hivyo kufanya watu wengi kupatumia kama eneo la matambiko, na inadaiwa kuwa waombaji walikuwa wakijibiwa maombi yao. Ikumbuke kwamba eneo hilo pia kulikuwa na Msikiti ambao ulizama ukiwa na waumini ndani yake.
Kufikia miaka ya 1960 baada ya kuanzishwa kwa kiwanda cha Tanganyika Packers palikuwa na njia ya kuleta ng'ombe kiwandani yaani (COW ways), wazungu waliita "cow ways" wakimaanisha njia ya ng'ombe, wazawa wakashindwa kutamka neno hilo na badala yake kutamka KAWE.
Vitongoji vilivyokuwa vinapakana na Kawe kwa kipindi hicho ni pamoja na Kwa Mussa Hassan ambako ni Msasani, Maiko Chain ambako sasa ni Mikocheni. Umbwelani ambako sasa ni pahala ilipo hosteli ya JWTZ, pia kwa Wakwama ambako sasa ni Ukwamani na upande wa Kaskazini walipakana na mashamba ya mkonge ya Asamali ambako sasa ni Mbezi Beach.
Kata ya Kawe inayo mitaa minne (04) kama ifuatavyo:-
Hali ya elimu katika Kata ni ya kuridhisha, hasa elimu ya awali, msingi, sekondari na uwepo wa vyuo vya elimu ya kati. Zote zinayo miundombinu muhimu inayohitajika kama vile umeme, maji, na mazingira tulivu.
Kata ya Kawe inazo shule za awali na za msingi saba (07) za serikali ambazo ni:
Kata ya Kawe inayo shule moja ya sekondari ya serikali ambayo ni Kawe Ukwamani.
Hali ya Afya katika Kata ya Kawe ni ya kuridhisha kwani ina Hospitali, Vituo vya Afya na Zahanati za serikali na binafsi.
Kata ya Kawe ina barabara 4 za kiwango cha lami ambazo ni Mwai Kibaki, Old Bagamoyo, Whitesands na barabara ya JK.
Barabara hizi zina mifereji inayotunzwa na Manispaa ya Kinondoni pamoja na TANROADS. Kadhalika Kata ya Kawe inazo barabara za vumbi za Mitaa ambazo zipo chini ya Manispaa.
Hali ya usafi wa mazingira katika Kata ya Kawe kwenye makazi ya watu, taasisi binafsi na za serikali inaridhisha. Mitaa yote inayo Wakandarasi wa ukusanyaji na uzoaji wa taka ngumu na malipo ya ushuru wa takataka ni kwa kutumia vifaa vya kielektroniki.
Mahusiano na ushirikiano katika Kata kati ya Mamlaka ya Serikali na wakazi ni mazuri, hali ambayo inarahisisha shughuli za kiserikali kama vile usafi wa wiki, katika Kata na mambo mengine.
Kata ya Kawe yapo maeneo ambayo ni makazi holela kwa mtaa wa Mzimuni na Ukwamani. Pia yapo baadhi ya maeneo ni ya kupimwa ambayo ni ya mtaa wa Mbezi Beach A na Mbezi Beach B na yapo maeneo ambayo hayajapimwa.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.