Kata ya Bunju ni miongoni mwa Kata kongwe ndani ya Manispaa ya Kinondoni. Jengo la ofisi ya Kata hii lilizinduliwa tarehe 29/06/2001 na kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa wa Mwaka huo ambaye ni Ndg. Fatma Juma Shomari.
Bunju imetokana na neno samaki anayeitwa jina la Bunju. Hapo awali wakazi wa eneo la Kata ya ya Bunju walikuwa wafugaji ambao walitekeleza shughuli zao za uvuvi katika bahari ya Hindi.
Eneo la kati la Kata ya Bunju lilikuwa na kijiji ambacho kulikuwa na vitongoji ambavyo mojawapo ni Mabwepande ambapo kwa sasa ni Bunju B. Lakini pia Mabwepande ilikuwa inasimamiwa na Kata ya Bunju na ilikuwa na Mitaa miwili ambayo ni Boko na Bunju A.
Kuna mchanganyiko wa makabila mbalimbali ndani ya Kata ya Bunju ikiwemo Wakwere, Wazaramo na Wandengereko.
Kata ya Bunju ina jumla ya mitaa sita (06) kama ifuatavyo:-
1. Mtaa wa Basihaya
2. Mtaa wa Boko
3. Mtaa wa Dovya
4. Mtaa wa Kilungule
5. Mtaa wa Mkoani
6. Mtaa wa Bunju A
Hali ya elimu katika Kata ni ya kuridhisha na wanafunzi wake hujitahidi kufikia lengo la ufaulu kwa asilimia zinazotakiwa. Kata hii inazo shule za awali, msingi na sekondari ambazo ni za serikali na za binafsi. Pia Kata ina vyuo vya elimu ya kati.
Kata ya Bunju inazo shule za awali na msingi saba (7) za serikali kama ifuatavyo: -
Kata ya Bunju inazo shule za awali kumi na tano (15) za binafsi kama ifuatavyo: -
Moga, Faith, Gosheni, Siya Modern, New Hazina, Abel Memorial, Prestige, Mt. Sinai, Stamarial Salome, Daystar, Locee, Turkish Maarif, Jubilation, Rev. Fr. Jagques, Mareisuvat.
Kata ya Bunju inazo shule tatu (03) za sekondari za serikali kama ifuatavyo: -
Kata ya Bunju inazo shule nane (08) za sekondari za binafsi kama ifuatavyo: -
Kata ya Bunju inavyo vyuo viwili (02) vya elimu ya kati vya binafsi.
Hali ya Afya katika Kata ya Bunju ni ya kuridhisha kwani ina Vituo vya Afya na Zahanati za serikali na binafsi.
Kituo cha Afya kilichopo ni kimoja ambacho ni cha serkikali ambacho kinaitwa Kituo cha Afya Bunju.
Kata ya Bunju ina Zahanati mbili (02) za serikali kama ifuatavyo: -
Kata ya Bunju ina Zahanati nane (08) za binafsi kama ifuatavyo: -
Tobson, St. Joseph, Sandary, Med Check, Agakhan Cilinic, Arafa Vigen, Burumawe Specilied Clinic Honest, Nyota Njema
Kata ya Bunju inazungukwa na barabara za lami nne ambazo ni Barabara ya Boko Chama kwenda Ununio na kutokea Kunduchi ambayo pia ina mifereji ya maji ya mvua, pia kuna barabara ya njia panda Mbweni kwenda Malindi Mbweni na ambayo pia ina mifereji na barabara nyingine kuanzia Kilungule kwenda Mbweni. Lakini pia Kata ya Bunju inapitiwa na barabara kubwa ya Bagamoyo kwa mitaa yote sita.
Hali ya usafi wa Kata ya Bunju ni wa kuridhisha, kwani mitaa yote sita inayo Wakandarasi wanaozoa taka na kusafirisha kwenda dampo.
Katika Kata ya Bunju, mdau mkubwa wa maendeleo ni kiwanda cha saruji cha Wazo ambacho mara kadhaa kimekuwa kikisaidia maendeleo katika mitaa ya Basihaya na Boko hasa katika kusaidia vifusi vya barabara, vyandarua na mazingira. Wadau wengine wanaosaidia katika Kata ni pamoja na: BARRIEL SHELI, ATN SHELI, APC, OILCOM SHELI, GUDAL SHELI, TOOTHPICK INDUSTRY LTD, DSN ENERGY (T) LTD (KIWANDA CHA MKAA), COLD BREWERIES ARIES, PRODUCT AZURA KIWANDA CHA POMBE), KIWANDA CHA GYPSUM.
Kata ya Bunju inajivunia hasa katika miradi ya elimu kwani pamoja na kuwa na shule nne za msingi na shule mbili za Sekondari bado imeanzisha ujenzi mpya wa shule ya msingi katika mtaa wa Mkoani.
Hali ya maendeleo ya watu na makazi inakua kwa kasi kwa kuwa watu wengi wamejenga nyumba za kisasa hasa katika eneo la mradi wa viwanja 2000 (Bunju Beach), na eneo la Boko beach ambako kuna miundombinu yote ya mipangomiji.
Pia katika maeneo yasiyopimwa ujenzi unafanyika kwa kasi.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.