Eneo la Kata ya Mbezi Juu hapo awali lilikuwa ni eneo ambao lilikuwa shamba la Mkonge na wakazi wake wengi walitokana na kabila la Wamakonde.
Asili ya jina la Mbezi Juu limetokana na jiografia yake ambayo ni ya milima na mabonde na hivyo kupelekea madhari yake kuonekana kuwa juu sana.
Kata ya Mbezi Juu imetoka kwenye ubavu wa eneo la Kawe ambapo mwaka 2009 iligawanywa na kupatikana Kata ya Mbezi Juu. Kata hii inakadiriwa kuwa na wakazi takribani 41,821
Kata ya Mbezi Juu ina jumla ya mitaa mitano (05) ya Kiserikali ambayo ni: -
Hali ya elimu katika Kata ni ya kuridhisha, hasa elimu ya awali, msingi, sekondari na uwepo wa vyuo vya elimu ya kati.
Kata ya Mbezi Juu inayo shule moja ya awali ya binafsi ijulikanayo kwa jina la Kyomo
Kata ya Bunju inazo shule tano (05) za msingi za serikali na za binafsi kama ifuatavyo: -
Kata ya Bunju inazo shule tano (05) za sekondari za serikali na za binafsi kama ifuatavyo: -
Kata ya Bunju inavyo vyuo vitatu (03) vya elimu ya kati vya binafsi kama ifuatavyo: -
Hali ya Afya katika Kata ya Mbezi Juu ni ya kuridhisha kwani ina Zahanati ya serikali na za binafsi.
Zahanati zilizopo katika Kata ya Mbezi Juu ni 5 ambapo 1 kati ya idadi tajwa ni ya serikali inayojulikana kwa jina la Zahanati ya Ndumbwi. Zahanati za binafsi ni: SUPER SPECIALIZED CLINIC, KETO, GEORGE na TAIFO.
Hali ya miundombinu bado ni mibovu, barabara nyingi ni za vumbi kwa hiyo wakati wa mvua miundombinu hiyo inakuwa sio rahisi kupitika. Barabara za mitaa yote hakuna ambayo ni ya kiwango cha lami, zaidi ya barabara kubwa ambayo inanzia Tangibovu kwenda Goba.
Mahusiano na wadau wa maendeleo katika ngazi ya Kata ikiwemo kampuni binafsi n.k ni mazuri sana kwani wamekuwa wanasaidia sana kwenye shughuli mbalimbali za kiserikali na kijamii kwenye nyanja za maendeleo.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.