Kata hii ilizaliwa kutokana na mgawanyiko wa Kata ya Msasani mwaka 2000. Jina Mikocheni lilipatikana wakati ikiwa Kata ya Msasani kuna mti wa matunda ulikuwa katika eneo aliloishi mzungu mmoja ambaye alikuwa akiitwa MICHAEL CHEN wakazi wa eneo hilo wakashindwa kuita jina hilo wakawa wanaita Mikocheni.
Kata ya Mikocheni ina jumla ya mitaa sita (06) ya Kiserikali ambayo ni: -
Hali ya elimu katika Kata ni ya kuridhisha, hasa elimu ya msingi, sekondari, vituo vya kulea watoto wadogo pamoja na uwepo wa vyuo.
Kata ya Mikocheni inazo shule za awali na za msingi kumi na moja (11) ambapo kati ya hizo 2 za serikali na 9 za binafsi.
Kata ya Mikocheni inazo shule za sekondari nne (04) ambapo 1 ni ya serikali na 3 ni za binafsi.
Hali ya Afya katika Kata ya Mikocheni ni ya kuridhisha kwani ina Zahanati na Vituo vya Afya vya serikali na binafsi.
Kata ya Mikocheni ina Zahanati mbili (02) moja ni ya serikali inayoitwa JS Babhra na moja ni ya binafsi.
Hali ya miundombinu ya barabara Kata ya Mikocheni ni ya kuridhisha kutokana na kuwa na mtandao mkubwa wa barabara za kiwango cha lami wenye urefu wa kilomita 40 na chache ni za kiwango cha changarawe ambazo asilimia kubwa zipo katika hali nzuri inayopitika katika misimu yote ya mwaka.
Mahusiano ya wadau wa maendeleo na uongozi wa Kata na mitaa ni mazuri, kwani wako mstari wa mbele kuchangia shughuli za kijamii na miradi ya maendeleo.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.