Kata hii ilizaliwa kutokana na mgawanyiko wa Kata ya Makumbusho. Kata ya Mwananyamala imeanzishwa miaka ya 1990, neno Mwananyamala lilmetokana na lugha ya Kizaramo ikiwa na maana mtoto nyamaza sababu ya jina hili ni tahadhari iliyokuwa ikitolewa kwa watoto kutokupiga kelele wala kulia wakati wakipita kwenye msitu wa Kijitonyama ambao ulikuwa na wanyama wakali na wapole.
Kabla ya mgawanyiko wa eneo la sasa la Kata ya Mwananyamala ilikuwa ni mashamba ya mpunga. Wenyeji wengi walikuwa ni wakulima na wafugaji. Kuna mchanganyiko wa makabila mbalimbali ambayo ni Wazaramo, Wapogoro, Wamakonde na Wayao.
ASILI YA JINA LA MWANANYAMALA; zamani Mwananyamala ilikuwa ni eneo moja na Kata za Makumbusho na Kijitonyama. Kulikuwa na msitu mkubwa na bwawa ambalo mpaka sasa lipo katika Kata ya Kijitonyama. Katika eneo la bwawa hilo na msitu huo kulikuwa na wanyama wakali walionekana na wasioonekana na kulikuwa na njia ambayo wananchi walikuwa wakipita kwenda kwenye shughuli zao mbalimbali ikiwemo kilimo katika maeneo ya Mwenge na kwingineko, hivyo wakati wakipita maeneo hayo walikuwa na tahadhari kubwa ya kutopiga kelele na hasa watoto walitahadhirishwa kutolia.
Mtoto nyamaza (Mwan- nyama) Mwana ni mtoto na Nyamala ni Nyamaza. Miaka ya 1990, Kata ya Mwananyamala ilikatwa na kuzaa Kata ya Makumbusho na Kiitonyama.
Kata ya Mwananyamala ina jumla ya mitaa saba ya Kiserikali ambayo ni: -
Hali ya elimu katika Kata ni ya kuridhisha, hasa elimu ya msingi, sekondari, vituo vya kulea watoto wadogo pamoja na uwepo wa vyuo.
SHULE ZA AWALI:
Kata ya Mwananyamala inazo shule za awali saba (7) ambapo kati ya hizo 4 za serikali na 3 za binafsi.
Hali ya Afya katika Kata ya Mwananyamala ni ya kuridhisha kwani ina Zahanati na Vituo vya Afya vya serikali na binafsi.
Kituo cha Afya kilichopo ni kimoja ambacho ni cha binafsi kinaitwa Kinondoni kwa Mvungi.
Zahanati zilizopo katika Kata ya Mwanayamala ni 3 ambapo 1 kati ya idadi tajwa ni ya serikali iitwayo Kambangwa na 2 ni za binafsi zinazojulikana kwa majina ya Msisiri B na KBDS Msolomi.
Asilimia kubwa ya barabara za Kata ya Mwananyamala zimejengwa kwa kiwango cha lami na changarawe. Barabara ya Mwinjuma kutoka studio (Ally Hassan Mwinyi Road hadi Mwananyama A urefu wa kilomita 4, barabara ya Dunga kutoka Biafra hadi mzunguko wa Peace urefu wa kilomita 2.5, barabara ya Ally Hassn Mwinyi bonde la Mkwajuni hadi Morocco. Morocco hadi Victoria.
Mahusiano ya wadau wa maendeleo na uongozi wa Kata na Mitaa ni mazuri, kwani wako mstari wa mbele kuchangia shughuli za kijamii na miradi ya maendeleo. Mfano; OSHA, VODACOM T, LTD, CRDB n.k.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.