Kata ya Mabwepande ilianzishwa 2010 kwa kupunguzwa eneo la kiutawala katika Kata ya Bunju na kuanzisha mitaa mipya mitano inayounda Kata ya Mabwepande. Jina Mabwepande ilitokana na maneno ya Kizaramo ambayo tafsiri yake ni mapande ya mawe (Marugwepande) yaliyokuwa yanapatikana kwenye Hifadhi ya Msitu wa Pande.
Kata ya Mabwepande inayo mitaa mitano (05) ambayo ni: -
Hali ya elimu katika Kata ni ya kuridhisha, hasa elimu ya msingi, sekondari, vituo vya kulea watoto wadogo pamoja na uwepo wa vyuo.
Kata ya Mabwepande ina shule za awali za Serikali nne ambazo: -
Pia Kata ina shule za awali za binafsi 90.
Kata ina shule nne za sekondari za Serikali ambazo ni: -
Pia Kata ina shule tano za sekondari za binafsi ambazo ni: -
Kata ya Mabwepande ina chuo 1 cha Serikali ambacho ni chuo cha kilimo Malolo na vyuo 2 vya binafsi ambavyo ni chuo cha Mazingira Bunju B na Tuwepende watoto.
Hali ya Afya katika Kata ya Mabwepandei ni ya kuridhisha kwani inayo hazina ya kutosha ya Hospitali, Vituo vya afya pamoja na Zahanati za serikali na binafsi. Kata ya Mabwepande ina Hospitali 1 ya serikali ambayoni Hospitali ya Wilaya ya Mabwepande na Hospitali mbili za binafsi ambazo ni Heameda na Hans Magaya.
Kata ya Mabwepande ina Zahanati mbili (2) za serikali ambazo ni Zahanati ya Mabwepande na Mbopo na Zahanati tatu (3) za binafsi ambazo ni Zahanati ya Upendo, Honest na Diason.
Kata ya Mabwepande ina barabara za udongo zinazopitika kwa msimu mmoja na msimu mwingine kupitika kwa taabu. Muonekano wa Kata ya Mabwepande ni muinuko na mabonde ukiwa umepitiwa na mto Mpiji upande wa Magharibi mwa Manispaa ya Kinondoni. Hata hivyo Kata ina barabara moja ya lami inayokwenda Bagamoyo yenye urefu wa kilometa 2.5
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.