Kata ya Kinondoni ni miongoni mwa Kata 20 zilizomo ndani ya Manispaa ya Kinondoni.
Kata ya Kinondoni ilianzishwa mwaka 2000 baada ya Kata Hananasif kugawanywa. Asili ya jina la Kinondoni linatokana na jina la mtu mmoja miaka ya nyuma ambaye alikuwa akiitwa KILONDONI mwenye asili ya kabila la Wanyamwezi ambaye alikuwa ni mkulima wa mpunga katika mashamba eneo la Biafra ambapo ndipo kulikuwa na majaruba ya mpunga.
Kutokana na umaarufu wa Bwana KILONDONI watu wakawa wamasema tunaenda kwa bwana KILONDONI ndipo likazalliwa jina la Kionondoni sababu watu wengi walikuwa wanashindwa kutamka KILONDONI wakawa wanatamka KINONDONI, hivyo kupekelekea jina la KINONDONI kuzaliwa.
Kata ya Kinondoni ina jumla ya mitaa minne (4) ya Kiserikali ambayo ni: -
Hali ya elimu katika Kata ni ya kuridhisha, hasa elimu ya msingi, sekondari, vituo vya kulea watoto wadogo pamoja na uwepo wa Chuo cha Elimu ya Juu.
Kata ya Kinondoni ina shule moja ya awali na msingi ya serikali ijulikano kwa jina la shule ya msingi Kumbukumbu.
Kata ya Kinondoni ina shule mbili (02) za awali na msingi ya serikali kama ifuatavyo: -
Kata ya Kinondoni ina shule tatu (03) za sekondari za binafsi na shule moja ya serikali.
Kata ya Kinondoni ina Chuo kimoja cha Elimu ya Juu kijulikanacho kwa jina la Chuo Kikuu Huria.
Hali ya Afya katika Kata ya Kinondoni ni ya wastani kwani ina jumla ya Hospitali na Vituo vya Afya vya binafsi
Kata ya Kinondoni ina jumla ya Hospitali sita (06) za binafsi kama ifuatavyo: -
Kata ya Kinondoni ina jumla ya Zahanati tatu (03) za binafsi kama ifuatavyo: -
Hali ya miundombinu ya barabara katika Kata ya Kinondoni inaridhisha.
Mahusiano na wadau wa maendeleo katika ngazi ya Kata ikiwemo kampuni binafsi n.k ni mazuri sana kwani wamekuwa wanasaidia sana kwenye shughuli mbalimbali za kiserikali na kijamii kwenye nyanja za maendeleo.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.