Kata ya Msasani ilikuwa inajulikana kwa jina la Mikoroshoni ambalo lilitokana na uwepo wa mikorosho mingi kwa wakati huo. Asili ya jina la Kata ya Msasani inasadikiwa kuwa ni kutokana na mtu maarufu aliyeishi maeneo hayo kipindi hicho aitwaye Mussa Hassan, na kutokana na wenyeji wa eneo hilo ambao walikuwa ni kabila la Wamakonde kushindwa kutamka kwa usahihi jina Mussa Hassan na kutamka Mucha Hachani na mwisho watu wakaanza kutamka Msasani.
Kata ya Msasani ina mitaa mitano (05) kama ifuatavyo:-
1. Mtaa wa Oysterbay
2. Mtaa wa Masaki
3. Mtaa wa Bonde la Mpunga
4. Mtaa wa Makangira
5. Mtaa wa Mikoroshoni
Hali ya elimu katika Kata ni ya kuridhisha, hasa elimu ya awali, msingi na sekondari za serikali na binafsi.
Kata ya Msasani inazo shule za msingi za serikali tano (05) ambazo ni
Shule zote hizi zina miundombinu ya maji safi na umeme. Shule ya msingi Oysterbay imepandishwa daraja na kuwa shule ya mchepuo wa kiingereza "English Medium". Aidha kuna vitengo vya kuhudumia watoto wenye mahitaji maalumu (Disabilities), katika shule ya msingi Msasani A na Mbuyuni.
Kata ya Msasani pia ina shule moja ya awali ya binafsi ijulikanayo kwa jina: Lady Chesham.
Kata ya Msasani inazo pia shule tisa za msingi za binafsi ambazo ni:-
Kata ya Msasani inayo shule moja ya sekondari ambayo ni ya serikali iitwayo Oysterbay.
Kata ya Msasani inazo pia shule za sekondari za binafsi tano kama zifuatazo;-
Kata ya Msasani ina Chuo cha Elimu ya Kati cha Serikali kimoja (1) ambacho ni Chuo cha Tanesco Masaki. Vilevile kuna chuo kimoja cha binafsi ambacho ni Don Bosco VTC.
Hali ya afya katika Kata ya Msasani ni ya kuridhisha kwani inayo hazina ya kutosha ya Hospitali, Vituo vya Afya pamoja na Zahanati za serikali na binafsi.
Hali ya miundombinu ya barabara Kata ya Msasani ni ya kuridhisha kutokana na kuwa na mtandao mkubwa wa barabara za kiwango cha lami na chache ni za kiwango cha changarawe ambazo asilimia kubwa zipo katika hali nzuri zinazopitika katika misimu yote ya mwaka.
Usafi wa mazingira wa Kata hii ni wa kuridhisha kwani kila Mtaa una Wakandarasi wa usafi wanaozoa taka kwa wakati na hutumia mashine za kielektroniki.
Mahusiano ya wadau wa maendeleo na uongozi wa Kata na Mitaa ni mzuri, kwani wako mstari wa mbele kuchangia shughuli za kijamii na miradi ya maendeleo.
Mradi wa kujivunia katika Kata ya Msasani ni ujenzi wa mfereji mkubwa wa maji ya mvua kutoka Mayfair hadi baharini ambao unasaidia kuondoa kero ya mafuriko katika Kata ya Msasani.
Kata ya Msasani eneo lake kubwa limepimwa na sehemu ndogo ya makazi holela ambako hakujapimwa hivyo kupelekea watu kupima wenyewe kunakoleteleza changamoto ya miundombinu ya barabara za mitaa.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.