Kata ya Makongo ni miongoni mwa Kata 20 za Manispaa ya Kinondoni. Kata hii imetokana na Kata ya Kawe. Asili ya jina Makongo ni aina ya miti ya kujengea (Makongo) ambayo ilikuwa inatumiwa na wenyeji wa eneo hilo ambao walikuwa ni Wamatumbi na Wangindo. Kata ya Makongo imepakana na Manispaa ya Ubungo.
Kata ya Makongo ina jumla ya mitaa minne (04) ya Kiserikali ambayo ni: -
Hali ya elimu katika Kata ni ya kuridhisha, hasa elimu ya awali, msingi, sekondari na uwepo wa chuo.
Kata ya Makongo inazo shule za msingi tatu (03) za serikali kama ifuatavyo: -
Kata ya Makongo ina shule za awali za binafsi kumi (10) kama ifuatavyo: -
Kata ya Makongo inazo shule za msingi tatu (03) za binafsi kama ifuatavyo: -
Kata ya Makongo inazo shule mbili (02) za sekondari za serikali kama ifuatavyo: -
Kata ya Makongo inazo shule mbili (02) za sekondari za binafsi kama ifuatavyo: -
Kata ya Makongo ina Chuo Kikuu kimoja cha serikali kinachojulikana kwa jina la Chuo Kikuu Ardhi.
Hali ya Afya katika Kata ya Makongo ni ya kuridhisha kwani ina Hospitali na Zahanati za serikali.
Kata ya Makongo ina Hospitali moja ya rufaa ya mama na mtoto inayomilikiwa na jeshi inayojulikana kwa jina la Benedicoy.
Kata ya Makongo ina Zahanati tatu za serikali kama ifuatavyo: -
Hali ya miundombinu ya barabara katika Kata ya Makongo ni ya kuridhisha. Hali ya miundombinu sio rafiki katika mtaa wa Makongo Juu, kwa kuwa maeneo yake yana mwinuko.
Mahusiano ya wadau wa maendeleo na uongozi wa Kata na mitaa ni mazuri, kwani wako mstari wa mbele kuchangia shughuli za kijamii na miradi ya maendeleo.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.