Kata ya Kigogo ni miongoni mwa Kata 20 za Manispaa ya Kinondoni. Asili ya jina Kigogo ni uwepo wa gogo lilokuwepo maeneo ilipo Randa bar kwa sasa ambalo lilikuwa na asili ya maji yaliyopatikana hapo.
Eneo hilo pia lilitumika kwa ajili ya matambiko na wenyeji wa eneo hilo ambao asili yao ni Wazaramo. Kwa sasa gogo hilo halipo tena.
Kata ya Mzimuni ina jumla ya mitaa mitatu (03) ya Kiserikali ambayo ni: -
Hali ya elimu katika Kata ni ya kuridhisha, hasa elimu ya msingi na sekondari kwa uwepo wa shule za serikali na binafsi.
Kata ya Kigogo inazo shule za msingi nne (04) za serikali kama ifuatavyo: -
Kata ya Kigogo inazo shule za msingi mbili (02) za binafsi kama ifuatavyo: -
Kata ya Kigogo inayo shule moja ya sekondari inayojulikana kwa jina la shule ya sekondari ya Kigogo.
Hali ya Afya katika Kata ya Tandale ni ya kuridhisha kwani ina Kituo cha Afya cha serikali na Zahanati ya serikali na za binafsi.
Kata ya Kigogo ina Kituo cha Afya kimoja cha serikali kinachojulikana kwa jina la Kituo cha Afya Kigogo.
Kata ya Kigogo ina Zahanati moja serikali inayojulikana kwa jina la Zahanati ya Kigogo.
Kata ya Kigogo ina Zahanati tano (05) za binafsi kama ifuatavyo: -
Hali ya miundombinu ya barabara katika Kata ya Kigogo ni ya wastani. Barabara moja tu iliyo na lami iliyojengwa na mradi wa CIUP yenye urefu wa mita 300, barabara nyingine zote ni za vumbi za kuunganisha mitaa na hali yake siyo nzuri.
Mahusiano ya wadau wa maendeleo na uongozi wa Kata na mitaa ni mazuri, kwani wako mstari wa mbele kuchangia shughuli za kijamii na miradi ya maendeleo.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.