Kata ya Kijitonyama ilianza mwaka 2000, na asili ya jina lake ni mto ambao ulikua ukitumika kuoshea nyama baada ya kuchinjwa na mto huo ulikua umezungukwa na wanyama mbalimbali na hapo ndipo lilipotokea jina la KIJITO CHA WANYAMA na hatimae KIJITONYAMA.
Kata ina jumla ya mitaa nane (08) kama ifuatavyo:-
1. Mtaa wa Mpakani A
2. Mtaa wa Mpakani B
3. Mtaa wa Alimaua A
4. Mtaa wa Alimaua B
5. Mtaa wa Kijitonyama
6. Mtaa wa Mwenge
7. Mtaa wa Nzasa
8. Mtaa wa Bwawani
Kata ina jumla ya shule tano za msingi na moja ya sekondari ambazo zote ni za Serikali, na kiwango cha ufaulu wa wanafunzi katika shule zote hizo ni cha kuridhisha. Orodha ya shule hizo ni kama ifuatavyo:
Kata ya Kijitonyama inazo shule za mbili (2) za sekondari za serikali na mbili (2) za binafsi kama ifuatavyo: -
Kata ya Kijitonyana ina chuo kimoja cha elimu ya juu cha Serikli (Chuo cha Ustawi wa Jamii) na chuo kimoja cha elimu ya kati cha binafsi (Kilimanjaro Institue of Technology)
Kata ina jumla ya Zahanati mbili za Serikali ambazo hutoa huduma kwa wakazi wa Mitaa yote nane. Kwa ujumla hali ya afya hasa upatikanaji wa huduma za afya ni mzuri, kwani pamoja na vituo hivyo viwili bado Kata iko jirani kabisa na Hospitali ya Sinza Palestina pamoja na Hospitali ya Mwananyamala ambapo wananchi wanaweza kuonana na madaktari bingwa na kupatiwa huduma wanayostahili.
80% ya barabara za Kata ya Kijitonyama ni za vumbi.
Kata inao utaratibu mzuri wa kudhibiti taka ngumu zinazozalishwa majumbani pamoja na maeneo ya biashara, ambapo katika kila Mtaa kuna Mkandarasi anaezoa taka na kuzifikisha dampo.
Wakazi wa Kijitonyama kwa ujumla wao wamekuwa wakitoa ushirikiano mkubwa katika kuchangia shughuli mbalimbali za maendeleo.
Hali ya maendeleo ya watu na makazi ni nzuri, na hii imechangiwa na kuwepo na makampuni pamoja na taasisi, hali iliyoongeza mwingiliano wa watu na biashara kukua zaidi.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.