Kata ya Ndugumbi ilianza mwaka 2000 baada ya Kata ya Magomeni kugawanywa. Asili ya jina la Kata ya Ndugumbi ni kutokana na mzee maarufu aliyekuwa akiishi hapo ambaye yeye na ndugu yake walikuwa wanashirikiana na serikali kwa ukaribu kama wadau wa maendeleo katika utoaji wa maeneo ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya kijamii ikiwemo shule, makanisa na misikiti. Mfano eneo lililojengwa shule ya sekondari Turiani lilitolewa na ndugu hao wawili kusaidia ujenzi wa shule hiyo.
Ndugumbi ni mojawapo ya Kata za Wilaya ya Kinondoni katika Mkoa wa Dar es Salaam, Tanzania, yenye postikodi namba 14104 na kwa mujibu wa Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 Kata ya Ndugumbi ina jumla ya wakazi 32,862.
Kati ya Wakazi hao Wanaume ni 16,102, Wanawake ni 16,760. Idadi ya Kaya ni 10,577 ambapo wastani wa watu katika Kaya ni 3.1
Kata ya Ndugumbi ina eneo la ukubwa wa mraba 1.315KM (sqm) 0.508. Kadhalika Kata ya Ndugumbi ina Mitaa Minne ambayo ni Mpakani, Mikoroshini, Mpakani na Makanya.
MIPAKA YA KATA YA NDUGUMBI.
Upande wa Mashariki Kata ya Ndugumbi inapakana na Kata ya Magomeni, upande wa Magharibi Kata ya Ndugumbi inapakana na Kata ya Manzese kutoka Wilaya ya Ubungo, upande wa Kaskazini inapakana na Kata ya Tandale na upande wa Kusini inapakana na Kata ya Makurumla kutoka Wilaya ya Ubungo pamoja na Barabara ya Morogoro (Morogoro Road).
MIPAKA YA MITAA YA KATA YA NDUGUMBI.
MTAA WA MPAKANI.
Mtaa wa Mpakani ni miongoni mwa mitaa 4 iliyopo katika Kata ya Ndugumbi Manispaa ya Kinondoni. Mtaa wa Mpakani una jumla ya wakazi 11,760, kati ya hao ME 5,793, na KE 5,967 Jumla ya kaya ni 2,940. Shughuli kuu za Kiuchumi katika mtaa wa Mpakani ni biashara.
MIPAKA.
Kwa upande wa Mashariki mtaa wa Mpakani umepakana na Mtaa wa Kagera Mikoroshini na Magharibi umepakana na Kata ya Manzese, Kaskazini umepakana na kata ya Tandale na Kusini umepakana na barabara ya Morogoro.
MTAA WA MAKANYA.
Mtaa wa Makanya ni miongoni mwa mitaa 4 iliyopo katika Kata ya Ndugumbi Manispaa ya Kinondoni. Mtaa wa Makanya una jumla ya wakazi 4,942, kati ya hao ME 2,416, na KE 2,526 Jumla ya kaya ni 1,526. Shughuli kuu za Kiuchumi katika mtaa wa Makanya ni biashara.
HALI YA ELIMU
Jumla ya shule ni 5. Serikali 4 Binafsi 1
Hali ya Afya katika Kata ya Ndugumbi ni ya kuridhisha kwani Kata ina Kituo cha Afya cha serikali pamoja Zahanati za serikali na binafsi.
Kituo cha Afya kilichopo ni kimoja ambacho ni cha serikali kinaitwa Kituo cha Afya cha Magomeni.
Kata ya Ndugumbi ina Zahanati moja ya binafsi inayojulikana kwa jina la Zahanati ya Subi.
Hali ya miundombinu ya barabara ni ya wastani, kukiwa na barabara kadhaa zinazoitaji marekebisho madogo, pamoja na kuwekewa mitaro mizuri pembezoni mwa barabara. Kkwa upande wa barabara za lami kuna takribani kilomita 10 barabara za kiwango cha lami katika kata ya Ndugumbi.
Hali ya Mahusiano na wadau katika Kata ni ya kuridhisha kwani hushirikiana pamoja katika kuleta maendeleo .
Kata inayo miradi inayojivunia kwayo ambayo hutekelezwa kama ifuatavyo:-
Katika Kata ya Ndugumbi, mipangomiji ni ya wastani, lipo eneo la Bonde Mtaa wa Makanya Vigaeni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.