Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni ni moja kati ya Halmashauri tano (5) zinazounda Mkoa wa Dar es Salaam. Zingine ni Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, Ubungo, Kigamboni na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni ilianzishwa kwa Sheria ya Serikali (Mamlaka za Miji) sura ya 288 kupitia Tangazo la Serikali (Government Notice No. 4) ya mwaka 2000 na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kama chombo huru, hivyo kuipa mamlaka ya kuongeza ubora wa utoaji huduma kwa wananchi wake.
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni inapakana na Bahari ya Hindi kwa upande wa Mashariki, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa upande wa Kusini, Wilaya ya Bagamoyo kwa upande wa Kaskazini na Wilaya ya Ubungo kwa upande wa Magharibi. Halmashauri inaunganishwa na sehemu nyingine za miji na nchi kwa mtandao wa barabara za mawasiliano. Barabara kuu ni pamoja na barabara ya Morogoro, Bagamoyo, Kawawa, barabara ya Sam Nujoma, Mwai Kibaki na Ally Hassan Mwinyi.
Hali ya hewa ya Manispaa ya Kinondoni ni ya joto la wastani wa nyuzi joto 290C kwa mwaka. Kipindi cha joto huanzia kati ya miezi ya Oktoba hadi Machi, wakati kipindi cha baridi chenye kadirio la nyuzi joto 250C huanzia kati ya miezi ya Mei hadi Agosti na nyuzi joto 29 – 330C kwa miezi iliyosalia katika kipindi cha mwaka. Wastani wa mvua kwa mwaka ni mm 1,300 katika misimu miwili ambayo ni vuli miezi ya Oktoba – Desemba na Masika ambayo huanza miezi ya Machi – Mei.
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni ina ukubwa wa kilomita za mraba 321. Kwa mujibu wa Sensa ya Taifa ya idadi ya watu na makazi ya mwaka 2012, Manispaa ya Kinondoni ilikuwa na idadi ya watu wapatao 929,681. Kutokana na ongezeko la ukuaji wa idadi ya watu ya asilimia 5.0 kwa mwaka, Manispaa inakadiriwa kuwa na idadi ya watu wapatao 1,373,562 ifikapo mwaka 2020, hivyo kila kilometa ya mraba kuwa na ujazo wa watu 4,279.
Kiutawala Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imegawanyika katika Tarafa mbili (2) ambazo ni Kinondoni na Kawe, Kata ishirini (20) na Mitaa ni mia moja na sita (106) ya utawala. Idadi ya Majimbo ya Uchaguzi ni mawili (2) ambayo ni Majimbo ya Kinondoni na Kawe. Mkuu wa Wilaya ni Msimamizi Mkuu wa shughuli zote za Serikali katika Wilaya. Manispaa inaongozwa na Baraza la Madiwani lenye wajumbe ishirini na tisa (29) ambapo kuna Madiwani 26 na Wabunge 3 ambapo Mstahiki Meya ni Kiongozi Mkuu na Mkurugenzi wa Manispaa ni Mtendaji Mkuu kwa upande wa Serikali za Mitaa.
Majukumu hayo ni kama ifuatavyo:-
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.