Kata ya Hananasif ni miongoni mwa Kata 20 zilizomo ndani ya Manispaa ya Kinondoni. Asili ya jina Hananasif linatokana na jina la mzungu raia wa Kigiriki ambae alikuwa akiitwa HANANASIF na mmiliki wa mashamba wakati wa ukoloni. Jina la Hananasif lilipatikana mnamo mwaka 1986 baada ya wananchi kuvamia shamba hilo.
Kata ya Hananasif ina jumla ya mitaa mitano (5) mitano ya Kiserikali ambayo ni: -
Hali ya elimu katika Kata ya Hananasif ni ya kuridhisha, hasa elimu ya awali, msingi na sekondari.
Kata ya Hananasif inazo shule mbili (2) za awali za binafsi ambazo ni: -
Kata ya Hananasif inazo shule mbili (2) za msingi za ambazo ni:
Kata ya Hananasif ina shule moja ya sekondari ya serikali inayoitwa Hananasif sekondari.
Hali ya Afya katika Kata ya Hananasif ni ya kuridhisha kwani ina Vituo vya Afya vya binafsi na Zahanati ya serikali.
Kata ya Hananasif ina Vituo vya Afya vitatu vya binafsi.
Kata ya Hananasif ina Zahanati moja (1) ya serikali ambayo ni Zahanati ya Hananasif.
Kata ya Hananasif ina barabara mbili tu ambazo ni za kiwango cha lami zenye urefu wa kilometa mbili (02). Barabara nyingine ni za vumbi.
Mahusiano na wadau wa maendeleo katika ngazi ya Kata ikiwemo kampuni binafsi n.k ni mazuri sana kwani wamekuwa wanasaidia sana kwenye shughuli mbalimbali za kiserikali na kijamii kwenye nyanja za maendeleo.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.