Mradi wa Kituo cha kisasa cha Daladala eneo la Mwenge kilichopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni utasaidia kutatua changamoto za usafiri kwa kusogeza huduma za usafirishaji, kuboresha na kuweka mazingira mazuri ya miundombinu kwa jamii.
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni katika kuboresha huduma za jamii kwa wananchi na wafanyabiashara wa eneo la Mwenge na Wilaya kwa ujumla iliamua kuanzisha ujenzi wa kituo cha mabasi Mwenge kwa fedha za mapato ya ndani katika mwaka wa fedha 2019/2020-2022/2023.
Mradi wa kituo cha mabasi Mwenge unatekelezwa kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza mradi ulitekelezwa kwa Force Account chini ya Local Fundi kikosi cha Jeshi la Wananchi Na. 361 Rejimenti kwa gharama ya Tshs 7,033,575,688.00 gharama iliyotumika mpaka mradi unasimamishwa ni Tshs 1,905,373,174.43.
Awamu ya pili Halmashauri iliingia mkataba na Mkandarasi HEINAN INTERNATIONAL LTD ambaye ndiye mjenzi kwa gharama ya Tshs 9,810,000,000 na msimamizi wa mradi huu akiwa na mhandisi mshauri “CRYSTAL CONSULTANTS” kwa gharama ya Tshs 304,136,064.00. Utekelezaji umefikia asilimia 87 ambapo kazi zinazofanyika kwa sasa kwenye jengo la maduka na car service ni umalizaji (skimming, kuweka ceiling boards, tiles na kuweka fremu za madirisha). Jengo la msikiti kazi imekamilika.
Kituo cha mabasi kazi ya kuweka “bays” na kutengeneza barabara ya kutokea inaendelea.
Mkandarasi kalipwa pesa ya malipo kwa asilimia 26 ambayo ni Tshs 2,591,648,597.72. na malipo yaliyofanyika kwa Mhandisi mshauri ni Tshs 304,136,064.00 na mpaka sasa mradi huu umetumia jumla ya Tshs 4,801,157,835.72
Katika kukamilisha mradi huu kituo kitakua na majengo matatu ambayo ni jengo la biashara lenye sakafu tatu litakalokuwa na jumla ya maduka 128 kwa ajili ya wafanyabiashara, vyumba 11 vitakavyotumika kama ofisi za kukodi, vyumba 12 kwa ajili ya mama lishe, migahawa ya chakula miwili, dukala kuuza vyakula (min supermarket) moja na vyoo kila sakafu.
Pia kuna jengo la kuhudumia magari (car service) ambalo litakuwa na sehemu ya kutengenezea magari na bajaji pamoja na maduka mawili ya vifaa vya magari (spare parts).
Jengo la walinzi ni mojawapo ya mpango wa mradi huu. Licha ya kuwepo kwa majengo haya pia kuna mpango wa kuwepo kisima cha kuhifadhia maji safi (underground water tank) chenye uwezo wa lita za ujazo 70,000.00 (70m3)
Kituo hiki cha mabasi kitakuwa na uwezo wa kuhudumia daladala 100 kwa wakati mmoja, magari binafsi 85 na bajaji 60.
Mradi huu unatarajiwa kuingizia Manispaa ya Kinondoni mapato ya Tshs. 800,000,000.00 kwa mwaka utakapokamilika.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.