Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imefanikiwa kupangiwa fedha za Serikali Kuu kwa ajili ya miradi ya kimkakati kiasi cha shilingi 9,000,000,000.00 ili kuweza kutekeleza ujenzi wa miundombinu ya soko la Magomeni.
Lengo la Serikali ni kuboresha maeneo ya masoko pamoja na wafanyabiashara wake ikiwa ni mpango mkakati wa kuziboresha Halmashauri zake, kwa kuziwezesha kutekeleza miradi ya kimkakati inayoweza kuwaingizia kipato na soko la Magomeni kuwa sehemu ya mpango huo.
Mradi huu unatarajiwa kuboresha mazingira ya kufanya biashara kwa wafanyabiashara zaidi ya 600 katika Soko la Magomeni pamoja na kuiwezesha Manispaa na Serikali katika ukusanyaji wa mapato.
Mradi wa Soko la Kisasa la Magomeni ni miongoni mwa miradi 22 iliyopewa ruzuku na Serikali katika Mpango wa Awamu ya Kwanza wa kuziwezesha Mamlaka za Serikali za Mitaa kujitegemea kimapato ambapo zaidi ya shilingi bilioni 147 zilitolewa na Wizara ya Fedha na Mipango kwa ajili ya kutekeleza miradi hiyo.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.