Barabara ya Kilongawima – Kunduchi ina urefu wa km 2 na ni miongoni mwa 0barabara zilizo katika Fungu la pili zenye jumla ya urefu wa km 11 ikiwa na gharama ya Shilingi 28,978,993,880.51. Mkandarsi mjenzi wa Mradi huu ni “China Civil Engineering Construction Corporation (CCECC). Ujenzi wa Mradi huu ulianza rasmi tarehe 28 Oktoba 2017 na unatarajiwa kukamilika tarehe 28 Agosti 2019. Kwa ujumla kazi zinazoendelea kufanyika katika barabara hii ni ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami urefu wa km 2, ujenzi wa mifereji ya maji ya mvua wenye upana wa mita 1.1, ujenzi wa makalavati sita (6) yenye ukubwa wa mita 0.9 na urefu mita 10 (pipeculverts) kila moja, Ujenzi wa kalvati (Box culvert) lenye upana wa mita 2 na kina mita 1.2, Ujenzi wa kalvati (Box culvert) lenye matundu mawili (double cell) yenye upana wa mita 4 na kina mita 1.2 kila moja, uwekaji wa taa zinazotumia nguvu ya jua (Solar Street Lights) na ujenzi wa njia za watembea kwa miguu zenye upana wa mita 1.5.
Mradi huu unajengwa kwa gharama ya Shilingi Bilioni mbili, milioni mia tisa thelathini na tisa, laki sita sabini na tano, mia tano ishirini na saba (Shilingi 2, 939, 675,527.00) ambapo malipo yaliyofanyika mpaka sasa ni Shilingi Bilioni moja, milioni mia nane kumi na nane, laki sita tisini na mbili, mia tano thelathini na senti sita (Shilingi 1, 818, 692,530.06) Fedha hizo Mkopo kutoka Benki ya Dunia kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Manufaa ya Mradi huu wa Barabara ya Kilongawima – Kunduchi ni pamoja na;
PICHA ZA MRADI WA BARABARA YA KILONGAWIMA-KUNDUCHI
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.