Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kwa ushirikiano na Jiji la Hamburg nchini Ujerumani wamefanikisha ujenzi wa kiwanda cha kuchakata taka na kuzalisha mbolea mboji katika Kata ya Mabwepande kwa fedha za kitanzania shilingi 5.56 bilioni.
Kiwanda cha uchakataji taka kinatarajiwa kutengeneza tani hamsini mpaka mia moja za mbolea ya mboji kwa siku ambayo itakayotumika kuongeza ukuaji mzuri wa mimea na kurudisha rutuba kwenye udongo uliokosa virutubishi na kuharibika.
Faida zitakazopatikana na mboji inayotengenezwa na kiwanda hicho ni pamoja na kusaidia mimea kukua vizuri wakati wa ukame, kusaidia mzunguko wa hewa kwenye udongo, kupunguza uchafu unaotupwa kwenye madampo pamoja na kuzuia uchafuzi wa mazingira.
Kiwanda hiki pia ni sehemu ya mchango mkubwa katika maendeleo ya nchi yetu katika kipindi hiki cha mapinduzi ya viwanda ikiwemo utoaji wa ajira kwa vijana na kuwa mojawapo ya vyanzo vya mapato vya Halmashauri.
Kiwanda kitasaidia kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabia nchi yanayosababisha kupungua kwa mvua, ukosefu wa rutuba katika udongo, pamoja na matatizo mengine ya mazingira.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.