NI KWA KUSHIRIKIANA NA SHIRIKA LISILO LA KISERIKALI LA JHPIEGO KUPITIA MRADI WA "TUPANGE PAMOJA" LENYE OFISI ZAKE MIKOCHENI.
Zoezi hilo lililoendeshwa kwa siku tatu kwa kushirikiana na shirika la JHPIEGO limehusisha utoaji wa Elimu sahihi ya uzazi wa mpango, huduma ya uzazi wa Mpango kwa njia za muda mfupi ,na muda mrefu na za kudumu, sambamba na huduma hizo pia zimejumuisha upimaji wa saratani ya shingo ya kizazi, maambukizi ya vvu, pamoja na shinikizo la damu, kwa Kata tano Kati ya Kata ishirini(20), za Manispaa hiyo.
Akifafanua malengo ya zoezi hilo Mratibu wa huduma za Afya ya uzazi, na Mtoto wa Manispaa ya Kinondoni Bi.Edith Manase Mboga amesema lengo ni kuhakikisha elimu sahihi juu ya maswala ya uzazi wa mpango inawafikia wananchi bila kupotoshwa, ikienda sambamba na ongezeko la matumizi sahihi ya njia za uzazi wa mpango
Ameongeza kuwa kwa kushirikiana na shirika la JHPIEGO chini ya mradi wa "TUPANGE PAMOJA" wamehakikisha Elimu sahihi, huduma ya uzazi wa Mpango,ushauri na upimaji wa magonjwa hayo inatolewa bure kwa wananchi.
Katika zoezi hilo lililohusisha Kata ya Hananasif, Magomeni, Tandale, Kunduchi na Mwananyamala, mratibu huyo amewataka wananchi kuwa na utaratibu wa kutumia njia za uzazi wa mpango, kupima afya zao mara kwa mara ili kuweza kutambua muenendo wa mwili Kiafya na kuchukua hatua stahiki pindi inapohitajika.
Imeandaliwa na
Kitengo Cha Habari na Uhusiano
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.