Zoezi hilo la ugawaji wa hati za viwanja kwa wakaazi wa maeneo ya Nakasangwe ni kufuatia ukamilishaji wa upimaji viwanja 9741vya wananchi hao walioendeleza maeneo kiholela hali iliyopelekea tatizo sugu la uvamizi.
Zoezi hilo limetangazwa rasmi na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Daniel Chongolo alipokuwa akiongea na wananchi wa Nakasangwe, katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo viwanja vya shule ya msingi Nakasangwe.
Amesema kwa kuwamilikisha Wananchi maeneo yao kisheria kutapunguza na kumaliza kabisa migogoro ya ardhi iliyokuwa ikiwakabili siku za nyuma.
"Ninafahamu Katika kata hizi za pembezoni hususani Mabwepande kumekuwa na watu wachache wanaojishughulisha na uvamizi wa maeneo na kuwauzia Wananchi hali inayopelekea migogoro, Nipende tuu kuwakumbusha kuwa magereza zetu nchini zinahitaji nguvu Kazi, serikali haitokubali kuwaacha watu Hawa waendelee kusababisha migogoro kwenye maeneo yetu."
Naye mkuu wa Idara ya Ardhi na Mipango Miji Manispaa ya Kinondoni Ndg. Maduhu Kazi amesema ugawaji huo wa hati ni kufuatia utekelezaji wa maagizo ya Serikali yanayozitaka Manispaa kupima meneo yote yalioendelezwa kiholela.
Amesema viwanja vilivyopimwa ni 9741 ambapo kulikuwa na makundi ya wenye migogoro na wasio na migogoro na kuwataka wanachi kufahamu kuwa ugawaji wa hati unaoanza kesho utahusisha maeneo ambayo hayakuwa na changamoto za migogoro.
Katika hatua nyingine, Mhe.Chongolo ameagiza wataalamu wa Manispaa kuanza kupima mtaa wa Mbopo uliopo Kata ya Mabwepande ndani ya siku 14, na kuwataarifu wanachi wanaosababisha migogoro kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Zoezi la upimaji wa viwanja ni endelevu na litafanyika kwa awamu likihusisha maeneo yote yaliyoendelezwa kiholela.
Imeandaliwa na
Kitengo Cha habari na uhusiano
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.