Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mheshimiwa Saad Mtambule amewataka Wakurugenzi wa Makampuni ya Ulinzi kuzingatia majukumu na sheria katika kutekeleza majukumu ya ulinzi na usalama ikiwemo kuimarisha na kusimamia nidhamu, haki, weledi na uadilifu.
Ametoa kauli hiyo Juni 25, 2024 alipokutana na Wakurugenzi wa Makampuni ya Ulinzi Wilaya ya Kinondoni katika Ukumbi wa Police Officers' Mess kwa lengo la kujadiliana na kuweka mikakati juu ya kuendelea kuimarisha ulinzi. "Tumieni madaraka yenu vizuri katika kuilinda na kuipeleka mbele Wilaya ya Kinondoni".
Mhe. Mtambule amesema, kusiwepo na Kampuni ya ulinzi katika Wilaya ya Kinondoni ambayo haijasajiliwa."Kila Kampuni ya Ulinzi ihakikishe inasajiliwa kwa kuzingatia matakwa ya sheria na majukumu ya Kampuni". Vile vile, amewataka Wamiliki wa Makampuni ya ulinzi kutetea maslahi kwa kuepuka kufanya kazi bila ya mkataba pamoja na kuzingatia mchango wa vijana kwa kuangalia maslahi yao ikiwemo taratibu za ajira, mishahara na stahiki zao.
Pia, Mkuu wa Wilaya amewaasa kuwa na matumizi sahihi ya silaha na ikitokea kinyume na hapo watasitishiwa umiliki huo. " Ikitokea silaha zinatumika kinyume na utaratibu, sheria itachukuliwa na kuzuia umiliki wa silaha hizo". Amesisitiza, Mhe. Mtambule.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.