Waziri wa Ujenzi, Mheshimiwa Innocent Bashungwa, amewaagiza Wakandarasi nchini kuzingatia Usalama na Afya za Wafanyakazi wao mahali pa kazi.
Mheshimiwa Bashungwa aliagiza hayo Aprili 30, 2024 alipokuwa kwenye ziara ya ukaguzi wa miundombinu katika Wilaya ya Kinondoni. Alisema, "Wafanyakazi kuvaa kandambili wawapo kazini ni kinyume cha maadili na sio salama kwa afya zao."
Aidha, Mheshimiwa Bashungwa aliwataka Wakandarasi kutoa vifaa bora vya kujikinga na mafunzo kwa wafanyakazi wao kuhusu matumizi sahihi ya vifaa hivyo, kinyume chake watachukuliwa hatua kali za kisheria.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.