Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo, ameanza ziara yake leo na kukutana na wananchi wakazi wa Kata ya Mbezi Juu katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika ofisi za Kata ya Mbezi Juu ikiwa ni utekelezaji wa mikakati ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi katika ziara yake ya Kata kwa Kata.
Amesema huu ni wakati muafaka wa kukutana na wananchi katika Kata zao na kujua zipi changamoto zinazowakabili ikiwa ni pamoja na kutoa nafasi kwa wananchi kusikilizwa na kupatiwa majibu stahiki kutoka kwa wataalamu wa Manispaa.
"Nimeamua kufika katika maeneo yenu kuweza kusikiliza Changamoto zenu na kuzipatia ufumbuzi kwani najua kuna baadhi ya wananchi wanapata ugumu kufika ofisini kwangu kunieleza Changamoto zao." Ameongeza Mhe Chongolo.
Naye Diwani wa kata hiyo Mhe. Anna Lukindo amesema wamefurahishwan na uamuzi wa Mkuu wa Wilaya kufika kwenye Kata yao na kutatua changamoto mbalimbali zilizokuwa zikiwakabili wananchi zikiwemo za Ardhi, Barabara, Shule na masoko.
Katika ziara yake hii Mhe. Chongolo amefanikiwa kusikiliza kero zipatazo 38, na kuzipatia ufumbuzi kupitia wataalam alioambatana nao.
Ziara hii ni endelevu kwa Kata zote 20 za Halmashauri na itahusisha wataalam mbalimbali kutoka Halmashauri, Dawasco, TAKUKURU pamoja na Polisi.
Imeandaliwa na
Kitengo cha Habari na Uhusiano
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.