Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake ambaye pia ni Naibu Meya wa Manispaa na Diwani wa Kata ya Bunju Mhe. Kheri Misinga imetembelea Kata ya Tandale na Shirika lisilo la Kiserekali - NGO PHSRF kwa lengo la kuangalia utekelezaji wa Afua za VVU na UKIMWI.
Mhe. Misinga amesema dhana nzima ya ziara hiyo pia ni kuweka msingi imara na mpango mkakati wa jinsi ya kushirikiana kwa pamoja na mashirika hayo yasiyo ya Kiserekali katika kuhakikisha maambukizi ya VVU yanapungua kwa kiwango kilichokusudiwa hali itakayoleta tija kwa Taifa letu.
"Kamati ya Kudhibiti Ukimwi ya Manispaa hatukubaliani kabisa na uwepo wa maeneo hatarishi ikiwemo biashara isiyo halali na nina shauri Kamati husika zichukue hatua, lakini pia nipongeze sana Shirika la PHSRF kwa kazi nzuri wanayoifanya". Amesema Misinga.
Naye Mratibu wa Kudhibiti Ukimwi Manispaa ya Kinondoni Bi. Rhobi Gweso anashukuru kwa ushirikiano mkubwa kutoka kwa wadau wa Afua za UKIMWI na ameahidi kuendeleza ushirikiano huo katika jitihada za kudhibiti maambukizi ya VVU na UKIMWI katika Manispaa ya Kinondoni na kufikia lengo tarajiwa la ziro maambukizi ifikapo 2030.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.