#. Aipongeza Serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dr.John Pombe Joseph Magufuli kwa kuboresha miundombinu ya barabara na mifereji kata ya Kijitonyama.
#.Aupongeza uongozi mzima wa Manispaa ya Kinondoni, waalimu wa shule za Msingi za Manispaa, pamoja na wazazi kwa ufaulu wa asilimia 95.7, matokeo ya mtihani wa darasa la saba kwa mwaka 2018, na kuifanya Kinondoni kuwa ya Kwanza kimkoa, na ya tatu Kitaifa.
#.Atoa rai kwa wananchi kuwa makini na matapeli wanaotumia hati zao za nyumba kuombea mikopo na mwisho wa siku nyumba zao kupigwa mnada.
#.Ataka wananchi kuheshimu maeneo ya wazi, na kuacha kuvamia maeneo ya Serikali, kwani kwa kufanya hivyo ni uvunjagi wa sheria na hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.
#.Atoa siku saba kwa wakandarasi wanaoshughulika na uzoaji wa taka, kuhakikisha wanaboresha huduma hiyo, ili kuondokana na mrundikano wa taka uliopo kwenye maeneo yetu, unaoweza kuleta magonjwa ya mlipuko.
#.Ataka kufanyike utaratibu wa polisi kuhakikisha wanawakamata wanaume(wateja) wanaojihusisha na madada poa(changudoa),kama wateja wao kwani kwa kufanya hivyo kutawaondolea madada hawa kufanya shughuli hiyo haramu.
#.Asema Kinondoni imejipanga kuboresha masoko yake yote, ili kuwatengenezea wafanyabiashara mazingira mazuri ya kufanya biashara zao, na kuwataka kila mfanyabiashara kupatiwa kizimba kimoja na si vinginevyo.
Imeandaliwa na
Kitengo cha habari na Uhusiano.
Manispaa ya kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.