Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imetoa rai kwa wafanyabiashara ndani ya Manispaa hiyo kurudi kwenye maeneo yaliyopangwa na yanayotambulika na Manispaa hiyo kibiashara.
Rai hiyo imetolewa leo tarehe 28 Januari, 2023 na Katibu Tawala wa Manispaa ya Kinondoni Bi. Stella Msofe wakati wa zoezi la usafi lililofanyika Kata ya Mbezi Juu iliyopo Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam huku likiongozwa na viongozi mbalimbali wa Serikali pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Abbas Mtemvu na viongozi wa shina mkoani humo.
"Niwaombe wafanyabiashara kutoka maeneo ya Manispaa ya Kinondoni kurudi katika maeneo yao rasmi kama walivyokuwa wamepangwa na kuelekezwa kwani sasa hivi kumekuwa na tabia kwa baadhi ya wafanyabiashara hasa maeneo ya Tegeta kwa Ndevu wameanza kuweka biashara zao barabarani," amesema Bi. Msofe.
Lakini pia Bi. Msofe amewaomba wananchi wa Kata ya Mbezi juu na Wanakinondoni kwa ujumla kuwa na utamaduni wa kufanya usafi katika maeneo yao kila siku na wasisubiri hadi siku ya mwisho wa mwezi.
Imeandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini:
Manispaa ya Kinondoni
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.