Ni kauli yake Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh Paul Makonda alipokuwa akizindua jengo la utawala katika Sekondari ya Makumbusho Manispaa ya Kinondoni, lililojengwa kwa msaada wa ushirikiano kutoka ubalozi wa China , ikiwa ni mpango mkakati wa kuboresha Mazingira ya waalimu ya kufundishia nje ya bajeti ya Serikali.
Amesema msingi imara wa Mwalimu kufundisha ni kuhakikisha mazingira bora na rafiki yanakuwepo, na hasa kwa jamii ya kipato cha chini yenye dhamira ya dhati ya kuliendeleza gurudumu la maendeleo kuelekea uchumi wa Kati wa viwanda ambalo msingi wake ni elimu.
Aidha amewataka waalimu kuhakikisha wanatumia taaluma zao ipasavyo ili kuleta maadili ya watoto katika mstari ikiwa ni pamoja na kuwafundisha wanafunzi maswala ya usafi, nidhamu, usikivu, na kuepukana na makundi ya vishawishi ili tuweze kujenga Tanzania ya wasomi kuelekea uchumi wa kati wa viwanda
"Ukitaka kumsaidia mtu wa hali ya chini, maskini, msomeshee wanawe, kwani ndiko kuliko na ufunguo wa maisha " Amesisitiza Makonda
Naye Balozi wa China Nchini Tanzania Ndg Wang Ke, amesema nchi yake imedhamiria kushirikiana na Tanzania katika kuhakikisha sera ya Uchumi wa Kati wa Viwanda, pamoja na elimu bila malipo inafanikiwa, ikiwa ni pamoja na kuboresha mazingira ya waalimu katika kuhakikisha wanatoa zao bora la ufundishaji.
Hafla ya uzinduzi huo pia imehudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Ilala No. Sophia Mjema, Katibu tawala Mkoa wa Dar es salaam Bi Theresia Mmbando, pamoja na viongozi wa vyama na Serikali.
Imetolewa na
Kitengo cha Uhusiano na Habari.
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.