Waziri wa maji na Umwagiliaji Eng Gerson Lwenge (MB) ameonesha kufurahishwa na maziwa yanayotokana na Mbuzi aina ya Saanen kwa kuwa na uwezo mkubwa wa kutibu magonjwa mbalimbali katika mwili wa mwanadamu.
Hayo yamedhihirika leo alipozuru banda la Maonesho ya Nane nane la Manispaa ya Kinondoni lililoko katika maeneo ya Tungi Mkoani Morogoro.
Pale alipotembelea banda la mifugo ya Mbuzi na kukutana na Ndg Athuman Ullotu mfugaji wa mbuzi na kueleza faida zitokanazo na maziwa ya mbuzi hao aina ya Saanen
Katika maelezo yake Ndg Ullotu amesema maziwa ya mbuzi hao hutibu magonjwa mbalimbali kama vile Sukari, Kiharusi, Mgongo, vidonda vya tumbo, figo, mifupa na pia hupandisha cd 4.
Eng Gérson pia alitembelea vipando mbalimbali vya mboga za majani, bwawa la Samaki, teknolojia ya Hydrophonic fodder na kupata maelezo mafupi kuhusiana na wasindikaji wa vyakula, na watengeneza mvinyo.
Eng Gerson katika ziara yake ameambatana na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dr. Steven Kebwe, pamoja na Ali Hapi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam.
Yote haya na mengine mengi utayapata katika banda la Manispaa ya Kinondoni kwenye maonesho ya Nane nane lililoko Mkoani. Morogoro.
Imetolewa na
Kitengo cha Uhusiano
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.