Afisa Ustawi wa jamii wa Manispaa ya Kinondoni Bi. Azza Abdallah, amewataka wazazi na walezi kuweka ukaribu na ushirikiano kwa watoto.
Bi. Azza Abdallah ameyasema hayo leo Septemba 22, 2023, wakati wa maadhimisho ya siku ya lishe Kata ya Magomeni yaliyofanyika katika ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Magomeni.
Aidha Bi. Azza amesema kuwa tunaposisitiza kuhusu masuala ya lishe kwa watoto wetu tukumbuke kuwalinda dhidi ya mmomonyoko wa maadili unaokithiri kila uchwao.
Amesema kuwa baadhi ya athari ziwapatazo watoto wetu zinasababishwa na uzembe wa wazazi na walezi wa kutokuwa na ukaribu na ushirikiano kwa watoto.
"Muda mwingine mzazi unatakiwa kumchunguza mwanao ili kubaini kama ameshafanyiwa matendo maovu" ameongeza Bi Azza.
Kadhalika Afisa mtendaji wa Kata ya Magomeni Bi Kulthum Msimika amewaasa wazazi na walezi kuwa na mwendelezo wa kuzingatia lishe kwa watoto maana watoto wanalindwa kwa kupewa lishe bora na malezi mema.
Bi. Kulthum amesema kuwa kuna baadhi ya familia wanaandaa chakula vizuri/ lishe mda ambao Wazazi wapo tofauti na kile kinachoandaliwa watoto wakiwa pekee yao hususani mchana.
"Milo ya usiku mara nyingi inaandaliwa kwa ubora na ufanisi unaokidhi lishe bora lakini ile ya mchana haifuati taratibu hizo kwa sababu walaji ni watoto tu" amesema Bi Kulthum.
Naye Asha Ramadhani (CHW) mtoa huduma wa Afya ngazi ya jamii amesema kuwa wazazi na walezi wanatakiwa kuwa walinzi wa kwanza kwa watoto kwa kuzingatia lishe bora kwao na pia ulinzi dhidi ya mmomonyoko wa maadili.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.