Wazazi na walezi watakiwa kuzingatia makundi matano ya chakula pindi wanapotengeneza chakula cha watoto ili kupunguza magonjwa yatokanayo na lishe ikiwemo utapiamlo.
Hayo yamesemwa na Afisa lishe wa Manispaa ya Kinondoni Bi. Emiliana Daud ikiwa ni siku ya afya na lishe katika Kata ya Makongo kwa robo ya kwanza ya mwaka 2023/2024.
Aidha, Bi. Emiliana amewataka wazazi hao kuhakikisha watoto wao wanapata vitamini ya nyongeza inayotolewa mara mbili kwa mwaka ambapo vitamini hivyo husaidia katika ukuaji na kuongezeka kwa mtoto.
Sambamba na mafunzo hayo huduma za upimaji wa afya zilifanyika ikiwemo upimaji wa hali ya lishe kwa watoto, upimaji wa presha na uzito.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.