Ni agizo lake Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh.Daniel Chongolo, alipokuwa akiongea na wananchi wa Kata ya Makongo katika ziara yake aliyoifanya leo.
Amesema watendaji wa Kata na Mitaa wapo kwa mujibu wa sheria, na kazi yao kubwa ni kuisimamia kwa kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao ili yaweze kuleta tija kwa wananchi, na sio kuwachekea watu wanaovunja sheria kwani hawa wanatucheleweshea maendeleo.
"Watendaji wa Kata, simamieni watu wanaokiuka na kuvunja sheria, kwani wajibu wenu mkubwa pamoja na shughuli nyingine ni hiyo, watu hawa wanatucheleweshea maendeleo", Amesisitiza Chongolo.
Awali akisoma taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo pamoja na shughuli za Kata kwa Mh Chongolo, Afisa Mtendaji wa Kata hiyo Bi.Husna Nondo amesema Kata hiyo ina wakazi wapatao 43,796, ambapo wanaume ni 21,289 na wanawake ni 22,509.
Ameongeza kuwa kata yake inatekeleza jumla ya miradi minne ambayo ni mradi wa zahanati ya Changanyikeni, ujenzi wa usambazaji maji shule ya msingi Changanyikeni, umaliziaji wa maabara shule ya Sekondari Makongo na Ujenzi wa barabara ya Mtaa Makongo juu.
Bi Husna pia ameainisha Changamoto zinazoikabili Kata ya Makongo kuwa ni kutokuwepo na kituo cha Polisi, Changamoto ya zoezi la Usafi kwa baadhi ya Mitaa, eneo la shule kuwa na mabonde, na kutokuwa na shule ya Sekondari ya karibu.
Akijibu swali la ukosefu wa madawa katika zahanati, Mganga Mkuu wa Manispaa hiyo Dr. Festo Dugange amesema katika zahanati dawa hutolewa kutokana na sera na miongozo ya Serikali na katika ngazi hii dawa zinazotakiwa ni 33 tu, ambapo kwa zahanati za Manispaa ya Kinondoni dawa hizo hupatikana kwa asilimia 100%.
Katika ziara hiyo Mkuu huyo wa Wilaya amekagua mradi wa zahanati pamoja na barabara inayojengwa na TARURA.
Imeandaliwa na
Kitengo cha Uhusiano na Habari.
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.