Ni kauli yake Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe.Daniel Chongolo alipozuru Kata ya Kijitonyama ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kikazi yenye lengo la kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua.
Amesema watendaji wa Kata na Mitaa ndio nguzo na kiungo muhimu kati ya wananchi na uongozi katika kufikisha mahitaji na changamoto zinazowakabili, hivyo yawapasa kuwajibika ili waweze kutatua kero hizo na Halmashauri iweze kusonga mbele kwa maendeleo.
" Watendaji wa Kata na Mitaa huku chini wajibikeni, watumikieni wananchi, wekeni utaratibu mzuri utakaowawezesha kukutana na wananchi, kuwasikiliza na kuwatatulia kero zao, huo ndio uzalendo na uwajibikaji unaotakiwa." Amesema Chongolo
Ameongeza kuwa kwa kufanya hivyo kutapunguza migogoro na changamoto zisizo zalazima zinazosababisha kutoelewana wenyewe kwa wenyewe hali inayochelewesha au kukwamisha baadhi ya shughuli za Serikali ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa miradi ya maendeleo itakayoleta tija kwa Taifa letu.
Katika ziara yake hiyo ikiwa leo ni siku ya Pili amefanikiwa kusikiliza na kutatua kero takribani arobaini zikihusisha kelele za baa, masuala ya taka, masuala ya dada poa, masuala ya mipaka, unganishwaji kiholela wa maji taka, masuala ya mirathi, mifereji ya maji ya mvua, masuala ya wastaafu pamoja na kero zihusuzo Taasis kama vile TARURA, DAWASCO na Tanroad.
Kadhalika Mkuu huyo wa Wilaya leo ametembelea Kata ya Kijitonyama eneo la Mwenge pamoja na ujenzi wa madarasa kumi katika shule ya Sekondari kijitonyama ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kikazi katika kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua.
Ziara hii imehudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo wenyeviti wa Serikali za Mitaa, TARURA, DAWASCO na kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya.
Imeandaliwa na
Kitengo Cha Habari na Uhusiano.
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.